Tetesi: Pogba Kudai Pesa Zaidi United

Nyota wa Manchester United Paul Pogba alikuwa anahitaji kuondoka klabuni Manchester United, alisistiza kuwa angependa kukumbana na changamoto zingine mahali pengine. Lakini Mashetani Wekundu hawakutaka kumuacha asepe klabuni hapo.

Taarifa zinazobamba chini ya kapeti ni kuwa kama United wataendelea na msimamo wao wa kumbakiza klabuni hapo, basi watajikuta wanaingia gharama kubwa zaidi baada ya nyota huyu kutajwa kuwa anahitaji ongezeko la pesa anayolipwa klabuni hapo.

Taarifa za uhitaji wake wa kuondoka United ziligonga vichwa vya habari katika vyanzo vingi vya habari za michezo huku klabu za Real Madrid na Klabu yake ya zamani ya Juventus zikitajwa kuwa na uhitaji wa huduma yake.

Stori Kubwa Hapa!

Staa Paul Pogba anahitaji kuongezewa mshahara mara mbili zaidi kufikia kiasi cha paundi milioni 30 kwa mwaka. Mkataba wake wa sasa unamlipa paundi milioni 15 kwa mwaka.

Kwa kuwa hakufanikiwa kuondoka, itakuwa ni jukumu la Man United kuangalia uwezekano wa kuendelea kuwa naye huku wakimpa kile anachokihitaji klabuni hapo.

2 Komentara

    Km anajitoa wampe tu

    Jibu

    Anazingua pogba

    Jibu

Acha ujumbe