Unakumbuka Prince Alitoa Ofa Kuinunua Man United?

Baada ya familia ya Glazer kumiliki klabu ya Man United tangia mwaka 2005, wamekuwa wakipokea ofa kadhaa bila kufanya maamuzi magumu.

Hata hivyo, kila jambo linawezekana! Mambo yanaweza kubadiliika na tukashuhudia mabadiliko ya wamiliki wa klabu hii kongwe wakati ikiwa inaendelea kupambana kurejesha hadhi yake.

Stori kubwa wakati United wakiendelea kupambana kurejesha heshima yao EPL mapema mwaka jana 2021 ilikuwa Mwana Mfalme wa Saudi Arabia, Prince Mohammed Bin Salman alitoa ofa ya kuinunua klabu ya Man United.

Jarida la The Mirror, lilimtaja Prince Mohammed Bin Salman kuwa yupo tayari kufanya ununuzi wa klabu hiyo wakati familia ya Glazer wakiwa wamemiliki klabu hiyo kwa takribani miala 15.

Hata hivyo, wakati Prince Mohammed Bin Salman akihitaji kuwekeza kwenye klabu ya United, Familia ya Glazer pia inatajwa kuwa haikuwa tayari kuwa kwenye mpango wa kuiuza klabu hii. Familia ya Glazer imeonekana kupiga vilivyo suala la kuiuza klabu ya Man United.

Unakumbuka Prince Alitoa Ofa Kuinunua Man United?
The Glazers hawajaonesha utayari wa kuiuza klabu ya Manchester United.

Hiki kilikuwa kikwazo kwa kutimia kwa nia ya mwana wa mfalme kumiliki klabu ya United. Lakini wataalamu wa mambo wanasema kuwa ni suala la muda tu kabla ya timu hiyo kuuzwa kwa yeyote atakayeweza kuiendesha, na kuondoka mikononi mwa The Glazer ambao wanaonekana kuchokwa na mashabiki.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe