Tetesi za Soka

Baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba huenda kocha wa zamani wa klabu za Manchester United na Chelsea, Jose Mourinho akarudi kibaruani tena kufundisha soka ikisemekana akajiunga na miamba wa soka wa Ujerumani, Borussia Dortmund uvumi huo umekanushwa na Mkurugenzi wa klabu hiyo kwa kusema kwamba jambo hilo halina uhalisia na siyo rahisi kutokea.

Klabu ya Manchester imeanza kuhisiwa kumsajili nyota wa klabu ya Bayern Munich, Thomas Muller mbali na kuwepo kwa taarifa kwamba nyota huyo hawezi kuuzwa. United ambao wanafikiria namna ya kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji walionekana kuhusishwa sana na kumhitaji nyota huyo.

Baada ya kuwa kwenye kipindi kizito cha fununu na kwamba huenda United wangewasajili nyota wawili wa klabu ya Leicester City inaonekana malengo ya klabu hiyo yameanza kuporomoka kwa sasa na klabu hiyo wanasema hawana nia ya kuwasajili Chilwell na Maddison kwa sasa ila wanaangalia zaidi kujiimarisha kwa namna nyingine.

Matajiri wa klabu ya Manchester City wameweka wazi kwamba walikuwa hatarini kumkosa kocha wao wa sasa Pep Guardiola kipindi wanamfukuzia na kumhitaji awe mwalimu wa kikosi chao. Wanasema mbali na mazingira ya kiuwekezaji kikosini lakini pia walikuwa na ushindani kutoka klabu nyingine kama United ambao nao walikuwa wanahusishwa na kumhitaji sana mkufunzi huyo.

Sidibe ambaye anachezea klabu ya Everton kwa mkopo akitokea Monaco, klabu yake hiyo kwa sasa wanasema hawana nia ya kumrudisha kwenye viwanja vyao mara baada ya kuwepo na ofa ya nyota huyo kutoka katika klabu ya AC Milan. Raia huyo wa Ufaransa ilitakuwa arejee lakini kutokana na uhitaji wake nje ya klabu yake huenda asirejee ndani ya klabu yake hiyo.

Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United, Paul Scholes anadai kwamba anatamani sana nyota wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil asajiliwe na kikosi cha klabu yake hiyo ya zamani kutokana na kuwepo kwa uhitaji wa mchezaji wa aina yake katika eneo la katikati ambalo halijawa na muunganiko mzuri sana kwa anavyoona.

Mkurugenzi wa michezo wa Wolves anasema kwamba kwa sasa klabu yake hiyo haina nia ya kumtoa kwa mkopo nyota wao, Kevin Thelwell kwamba wao hawajashindwa kumtumia nyota huyo na bado ana nafasi ya kufanya mengi ndani ya kikosi chao hicho.

3 Komentara

    Hii itakuwa poa.

    Jibu

    Asnteh kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe