Tetesi zinasema Inter Milan watajiandaa kumuuza mlinzi Mslovakia Milan Skriniar, 25, kwa Tottenham kwa pauni milioni 45 mwezi ujao.

Tetesi zinasema Mlinzi wa kati wa Uholanzi Perr Schuurs, 21, aliyehusishwa na taarifa za kuhamia Liverpool, anasisitiza kuwa hayuko tayari kuondoka Ajax.

Tetesi zinasema Pochettino anadhaniwa kuwa yuko tayari kuhamia Paris St-Germain na kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel.

Tetesi zinasema West Ham wako katika mazungumzo na meneja David Moyes kuhusu kuongezwa kwa mkataba wake , ambao unamalizika msimu huu.

Zidane amepoteza imani na wachezaji wake kadhaa ikiwa ni pamoja na winga wa zamani wa Chelsea Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 29- ambaye ni mchezaji wa kimataifa kutoka Ubelgiji.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Zidane anaungwa mkono na bodi ya Real Madrid na wachezaji kwa sasa, lakini hali yake katika timu hiyo ya siku zijazo inaweza kuamliwa na mechi tatu zijazo za timu hiyo.

Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry atamtafuta mchezaji mwenza wa zamani katika timu ya Chelsea Ashley Cole kushikilia nafasi ya kazi katika utawala wake wa timu kama atateuliwa kuchukua kazi ya kudumu ya kocha Phillip Cocu.

Tetesi zinasema Meneja wa Tottenham Jose Mourinho anasema ni jukumu lake kuamua iwapo klabu hiyo itamuuza kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, mwezi Januari au la.

Newcastle wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu mchezaji wa Manchester United Brandon Williams huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 20- anayecheza safu ya nyuma-kushoto katika kikosi cha vijana waliochini ya umri wa miaka 21 cha England anaweza kupatikana kwa mkataba wa mkopo mwezi wa Januari.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema yeye pamoja na mkururugenzi wa masuala ya kiufundi Edu wanafanya mpango kwa ajili ya kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari na kile kinachoweza kuwa soko lisilotarajiwa.

Werder Bremen wameachana na mpango wa kumuuza kiungo wa kati Mkosovo Milot Rashica mwezi Januari licha ya taarifa kwamba Aston Villa wanaweza kurejelea nia yao kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 24.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Leicester wanaweza kumsajili mchezaji wa kati Mreno William Carvalho, 28, huku Real Betis wakipanga kumuuza Januari.

Kiungo wa kati na mshambuliaji wa Timu ya Ufaransa Houssem Aoaur, 22, ambaye alihusishwa na timu ya Arsenal katika msimu huu, anasema anafurahia kwamba aliendelea kubakia katika klabu ya Lyon.

Primia Ligi haitajaribu kutoa chanjo za Covid-19 kwa wachezaji wa soka kabla ya kutolewa kwa chanjo hizo kwa umma kwa watu wote.

Tetesi zinasema watangazaji wamejipanga kuendelea kutoa kelele bandia kwa ajili ya soka katika televisheni, licha ya kurejea kwa mashabiki.

Televisheni za Sky Sports na BT Sport zitatumia mchanganyiko wa kelele kutoka kwa mashabiki, ambazo zimekuwepo katika mechi tangu mechi ziliporejea viwanjani bila mashabiki mwezi Juni.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

23 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa