Tetesi zinasema Arsenal na Liverpool wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 24.

Mlinzi wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27, na mlinzi wa England Fikayo Tomori, 22, wanaweza kuondoka kwenye klabu hizo wakati wa kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari.

Tetesi zinasema Tottenham, Everton na Atletico Madrid wanamfwatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Napoli Arkadiusz Milik, 26 raia wa Poland.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.
 

West Ham wanamsajili mlinzi wa kikosi cha Denmark cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Frederik Alves Ibsen, 20, kutoka Silkeborg kwa gharama ya pauni milioni 1.2 mwezi Januari.

Tetesi zinasema Barcelona imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa kati Mfaransa France Ousmane Dembele kuhusu mkataba mpya , huku Manchester United nao wakiendelea kumsaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Manchester United wanapaswa kumfuta kazi meneja wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer na nafasi yake ichukuliwe na ama Mauricio Pochettino, Antonio Cone au Diego Simeone, anasema mmiliki wa wa zamani wa Crystal Palace Simon Jordan.

Wayne Rooney ameendelea kusema kuwa bado anaipendelea kuwa meneja wa kudumu katika klabu ya Derby County, licha ya mchezaji mwenzake wa zamani wa England John Terry kuhusishwa na kazi yake.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Arsenal wanatakiwa kumsajili mshambuliaji wa kati wa Crystal Palace raia wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28,anasema David Seaman, ambaye alishinda mataji matatu ya ligi na vikombe vinne vya FA akiwa na Gunners.

Meneja wa Tottenham Jose Mourinho, 57, anaamini kuwa bado ana miaka 15 hadi 20 iliyobaki katika kazi yake ya kufundisha, ikimaanisha kuwa anataka kuwa bado ni meneja wa soka akiwa na miaka 70 na zaidi.

Wakati huo huo, kiungo wa kati wa Arsenal Muruguay Lucas Torreira, 24, bado ana muda wa mchezo katika siku zijazo katika Gunners licha ya kucheza kwa mkopo katika Atletico Madrid, anasema Gilberto Silva, aliyeshinda taji moja la Primia Ligi na vikombe viwili vya FA Cups akiwa na Gunners.

Newcastle United wanataka kumsaini mlinzi wa Manchester United kutoka kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21-Brandon Williams, 20, ambaye bado hajaanza mchezo wa Primia Ligi msimu wa 2020-21.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa