Tetesi zinasema mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 27, amepata ofa za timu kubwa sita za ligi ya Epl, Manchester United, Liverpool, Chelsea, Tottenham, Manchester City na Arsenal.

Tetesi zinasema Manchester United inamfuatilia mlinzi wa Kiingereza wa Atletico Madrid Kieran Trippier, 30, huku Ole Gunnar Solskjaer akimuhitaji pia kwa ajili ya kumpa changamoto Aaron Wan-Bissaka, 23.

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 32, anaamini kuwa ataweza kupata klabu nyingine bora – lakini ana uwezekano wa kuondoka kabla ya msimu ujao.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Manchester United imeibuka kuwa kinara katika kinyang’anyiro cha kupata saini ya kiungo wa kati wa Argentina Thiago Almada, 19, wa Velez Sarsfield.

Tetesi zinaseama kiungo wa kati wa Liverpool, Mholanzi Georgio Wijnaldum, 30, amedokeza kuwa anasubiri klabu ichukue hatua kuhusu kuongeza mkataba wake.

Arsenal inaweza kulazimika kuharakisha uhamisho wa Dominik Szoboszlai wakati wa dirisha la Januari baada ya habari kuibuka kuwa Real Madrid wamepanga kutoa kitita cha fedha kwa ajili ya kiungo wa kati wa Hungary anayekipiga Salzburg.

Wadhamini wa shati wa Manchester United Chevrolet wanaamini itakuwa jambo la thamani kibiashara kusaidia kufadhili hatua ya kumrejesha, Old Trafford mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35.

 

Cristiano Ronaldo

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Leonardo ameondoa matarajio ya klabu kumsajili kiungo mchezeshaji wa Argentina Lionel Messi ikiwa mchezaji huyo wa miaka 33 ataondoka Barcelona mwakani.

West Ham ni miongoni mwa vilabu vingi vya England na Ureno vinavyomtolea macho mchezaji wa zamani wa Tottenham Marcus Edwards, winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 sasa anaichezea Vitoria Guimaraes.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

24 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa