Tetesi zinasema mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 23, ambaye mkataba wake unakamilika mwaka 2023, anatarajiwa kupata kitita kikubwa Manchester United mwaka ujao.
Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, na kiungo wakati wa Italia Federico Bernardeschi, 26, ni miongoni mwa wachezaji waliotolewa kwa Manchester United huku Juventus ikitazamia kufikia mkataba wa kumsajili tena kingo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27.
Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ameongeza matumaini ya kujiunga na Sami Khedira baada ya kuonesha ishara kuhusu uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Juventus na Ujerumani, 33.

Mlinzi wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 24, anafuatiliwa kwa karibu na Liverpool kabla ya dirisha la uhamisho kufunguliwa mwezi Januari na huenda akasajiliwa kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu.
Tetesi zinasema Inter Milan na Barcelona wanapigania saini ya Wijnaldum wa Liverpool.
Tetesi zinasema Sheffield United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, kwa mkopo mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.
Mesut Ozil anajiandaa kusalia Arsenal hadi mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu huu lakini kiungo huyo wa kati wa Ujerumani aliye na umri wa miaka 32-ananyatiwa na klabu kadhaa ikiwemo Fenerbahce.
Tetesi zinasema Ozan Kabak, 20, anayesakwa na Liverpool anakaribia kufanya uamuzi kuhusu hatma yake ya baadae lakini mchezaji huyo wa Schalke wa safu ya kati nyuma angependa kuhamia AC Milan.
Hatua ya kumsajili kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 29, imeisaidia Everton kupata mkataba wa kwanza wa biashara nchini Colombia na washirika wake wasmi wa mchezo wa kamari katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.
Mkataba wa kiiungo wa kati wa Tottenham na Portugal Gedson Fernandes, 21, unakamilika mwezi Januari, baada ya Benfica kuamua kukatiza mkataba wake wa mkopo, ambao ulitarajiwa kuendelea hadi mwisho wa msimu huu.
Tetesi zinasema Manchester City awanajiandaa kupokea ofa ya kumuuza Oleksandr Zinchenko, 24, ambao mkataba wake katika klabu hiyo imekamilika.
Kiungo wakati wa zamani wa West Brom James Morrison amepandishwa cheo kujiunga na kikosi cha kwanza cha wakufunzi wa Allardyce, klabu hiyo pia imemleta mlinzi wa zamani wa Middlesbrough na Tranmere Robbie Stockdale kama kocha wa kwanza.
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!
Tatu
Bora Ozil abaki arsenal maana sasahv wana hali mbaya
Mwanahamisi
Ozili jembe
Shakila mrope
Ozili ni mchezaji bora sana abaki tu asernal
Adelta
Ozil abaki tu
Issa
Rashdfold amekua mtu bora sasa united
Caroline
Asante kwa taarifa
Saupha mohamed
Namkubali sana ozil
Sarah
Abaki tu ozil
Hopemwaikuka
Itakua poa sana
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa poa akibaki
Dorophina
Rashford amekuwa mchezaji bora sana pale united
samiah
Abakietu
warda
Rashford yuko vizuri sana acha apate anachostail
aisha
Ozil mtu mbaya
neema hassan
Ozil jeshiiii