Tetesi zinasema kutimuliwa kwa kocha wa PSG Thomas Tuchel kumeathiri matumaini ya klabu ya Real Madrid kumsaini mshambuliaji Kylian Mbappe kutoka klabu hiyo ya Ligue 1.
Tetesi zinasema Atletico Madrid inajaribu kumsajili beki wa Arsenal na England mwenye umri wa miaka 23 Ainsley Maitland-Niles kwa mkopo mwezi Januari.
Beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso pia analengwa na Atletico Madrid, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akikosa fursa ya kukichezea kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya Stamford Bridge msimu huu.

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili beki wa kati mwaka ujao lakini hatajiunga katika kinyanganyiro cha kumsaini beki wa Austria David Alaba 28, ambaye kandarasi yake inaisha mwisho wa msimu.
Mkufunzi wa AC Milan Stefano Pioli anataka kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu, ambaye amehusishwa na Man United kusalia katika klabu hiyo huku mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiendelea.
Manchester City na Tottenham zinamfwatilia kiungo wa kati wa klabu ya Atalanta na Uholanzi mwenye umri wa miaka 29 Marten de Roon, ambaye aliwahi kuichezea klabu ya Middlesbrough mapema akianza kucheza soka.
Mkufunzi wa Feyenoord Dick Advocaat amefutilia mbali hatua ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Everton na Turkey Cenk Tosun, 29.

Tetesi zinasema Barcelona imepinga madai kwamba inataka kumsajili beki wa Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 28 Shkodran Mustafi.
Chelsea imejiunga na Manchester United katika kuonesha hamu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Ecuador Moises Caicedo 19, anayeichezea klabu ya Independiente del Valle.
Tetesi zinasema Napoli itasikiliza ofa za kiungo wa kati wa Uhispania Fabian Ruiz baada ya mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na mchezaji huyo.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???




Shakila mrope
Asant kwa taarifa meridian bett
Saupha mohamed
Good news
Rahmal
Shukrani kwa talifa
Ernest Kimeru
Ipo msiku Chelsea watamkumbuka Marcos Alonso
Lydia Emmanuel Magoti
Habari hipo poa
Hopemwaikuka
Zko poa ngoja tuone matokeo
warda
Daaa itakuwaje sasa