Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema Chelsea imeripotiwa kuanzisha mazungumzo na Bayern Munich kuhusu mpango wa kumsajili beki wa Bayern Munich Niklas Sule kwa dau la £25.9m.

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kwamba klabu hiyo itaongeza kandarasi ya Sule, lakini hilo litategemea hali yao ya kifedha.

Tetesi zinasema kocha wa zamani wa Watford na Westbrom, Nigel Pearson anakaribia kuchukua ukufunzi wa klabu ya Bristol City baada ya mazungumzo na klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza.

 

Tetesi zinasema Manchester United inafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua kipa wa AC Milan na Itali Gianluigi Donnarumma, 21.

Crystal Palace inamchunguza beki wa kati wa Juventus na Romania mwenye chini ya umri wa miaka 21 Radu Radu Dragusin, 19, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Tottenham na Newcastle.

Tetesi zinasema Liverpool huenda ikabadilishana kiungo wa kati wa Japan Takumi Minamino, 26, na winga wa Sevilla na Argentina Lucas Ocampos, 26.

Tetesi zinasema West Ham huenda ikachuana na AC milan katika msimu wa joto kumsajili mshambuliaji wa Sevilla na Morocco Youssef En-Nesyri, 23.

 

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, anatarajiwa kuanza mazungumzo mapya na Juventus katika kipindi cha siku chache zijazo.

Kipa wa Brighton Robert Sanchez, 23, ambaye anaweza kuichezea Uhispania au England , amepatiwa kura ya kuwa na imani naye na kipa anayemuenzi Iker Casillas, mchezaji wa zamani wa Uhispania .


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

6 Komentara

    Chelsea bwana kila siku wanasajili lakin hakuna kitu

    Jibu

    Zmekaa vzur ngoja tuone matokeo

    Jibu

    Safi sana Man U kwa maamuzi yao

    Jibu

    Tetesi zipo poa

    Jibu

    Ziko vizuri tetesi

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe