Tetesi zinasema Manchester City inafikiria kutoa zaidi ya £100m kuwanunua mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, na kiungo wa kati wa Marekani Giovanni Reyna, 18, mwisho wa dirisha la uhamisho.

Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, hayuko tayari kuingia mkataba mpya huku klabu hiyo ikiendelea kuhusishwa na Haaland.

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekiri kwamba amekuwa akiwasiliana na Haaland, ambaye alikuwa akimfunza wakati akiwa mkufunzi wa Klabu ya Molde.

 

Kounde: Guardiola Aliniahidi Kunichezesha.

Tetesi zinasema Manchester United haiko tayari kulipa dau la £68m kumnunua beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Jules Kounde.

West Ham itakabiliana na ushindani dhidi ya Leicester City iwapo wanataka kufanya uhamisho wa kiungo wa kati wa Man United Jesse Lingard 28 kuwa wa kudumu.

Manchester United inasema kwamba thamani ya Kipa wa England Dean Henderson ni £40m iwapo wataamua kumuuza mchezaji huyo.

Tetesi zinasema Klabu ya Norwich City inatumai kwamba itapokea £35m kwa kumuuza beki wa England Max Aarons, 21, ambaye analengwa na Manchester United.

Everton haijawasiliana na Norwich kuhusu mkataba wa Aarons na inatarajia ushindani mkali kutoka kwa Manchester United, Bayern Munich na Barcelona.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema beki wa Crystal Palace na Uholanzi Patrick van Aanholt ameanza mazungumzo na klabu isiojulikana iliofuzu katika ligi ya klabu bingwa.

Tetesi zinasema Manchester United haitatumia kifungu cha kuongeza kandarasi ya mwaka mmoja zaidi ya kiungo wake wa kati Juan Mata 32.

Klabu za ligi ya serie A Juventus, Inter Milan na Roma ziko tayari kumsaini Mata wakati atakapokuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu.

Sunderland itajaribu kumsaini beki wa Wolves na England Dion Sanderson, 21, kwa kandarasi ya kudumu mwisho wa msimu.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa