Tetesi za Soka Barani Ulaya.


 

Tetesi zinasema Manchester United inaweza kumsajili Paul Torres 24, kama watamkosa Jules Kounde, 22 ambaye ana gharama kubwa zaidi.

Tetesi zinasema meneja wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amevutiwa kuhamia Tottenham, kama klabu hiyo ya Primia Ligi itaachana na meneja wake Jose Mourinho.

Manchester United watatumia michezo yao 16 ya Ligi ya Uropa AC Milan kumfuatilia kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu, 27, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

 

Mkurugenzi mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema kuwa kabu hiyo ya Bundesliga italazimika kumuachilia mchezaji kwasababu za kifedha zilizosababishwa na janga la Corona.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, yuko tayari kubakia Tottenham kwa angalau mwaka mwingine mmoja zaidi.

Mgombea wa urasi wa klabu ya Barcelona Toni Freixa anadai kuwa anamakubaliano ya kusaini mkataba na wachezaji wawili wa ngazi ya juu wanaotaka kushinda taji la Ballon d’Or iwapo watachaguliwa.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Alexandre Lacazette, 29, ameonekana kuwa analengwa na klabu ya Ligue 1 Monaco msimu ujao.

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel amepewa ruksa na klabu kusaini mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund, anayesakwa sana na klabu mbali mbali.

 

Tetesi zinasema mlinzi wa timu ya Uhispania Hector Bellerin, 25, anaweza kuondoka Arsenal msimu huu kama sehemu ya makubaliano na meneja Mikel Arteta.

Liverpool wanamfwatilia mshambuliaji wa Real Madrid Mbrazili Rodrygo, 20, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka katika ligi ya La Liga kwa pauni milioni 50.

Kiungo wa kati wa timu ya Toronto FC Jahkeele Marshall-Rutty mwenye umri wa miaka 16 amezivutia timu kubwa za Ulaya, huku Manchester City, Chelsea, Manchester United, Bayern Munich na Juventus zikisema zinamuhitaji Mcanada huyo.

Kiungo wa kati wa Manchester City Mjerumani Ilkay Gundogan, 30, anasema Manchester United ilianza mazungumzo ya kusaini mkataba nae kuanzia Borussia Dortmund miaka miwili au mitatu kabla ya kuhamia katika City.


ENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Tetesi zinasomeka

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki

    Jibu

    Ziko vizuri tetesi

    Jibu

    Tetesi ziko poa

    Jibu

    Safiii

    Jibu

    Zko njema

    Jibu

    Hawa United kila siku wanataka kusajili hata sion wanacho sajili

    Jibu

Acha ujumbe