Tetesi za Soka Barani Ulaya.


 

Tetesi zinasema Barcelona wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32 japo itategemea na Lionel Messi kuendelea kusalia Camp Nou.

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer huenda akawauza wachezaji Jesse Lingard, 28, Juan Mata,32, Diogo Dalot 21 na Phil Jones, 29, kuongezea bajeti yake ya £80m msimu wa joto.

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc, amesema klabu hiyo imepatia kipaumbele kushinda Ligi ya Mabingwa kupitia Bundesliga wanapojitahidi kusalia na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kwa muda mrefu iwezekanavyo.

 

Tetesi zinasema Manchester City wamewasiliana na Sporting Lisbon kumhusu mlinzi wao Nuno Mendes wanapojiandaa kuitangulia Real Madrid katika juhudi za kumsajili nyota huyo Mreno aliye na umri wa miaka 18.

Tetesi zinasema Arsenal wanamtaka mlinzi wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Evan N’Dicka, 21, na wameomba kupewa maelezo kuhusu hali ya kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma,24.

Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez, 23, anaamini kuwa atasaini mkataba mpya na klabu hiyo, licha ya kile Muargentina huyo alichotaja kuwa changamoto kidogo za kifedha zinazokabili klabu hiyo ya Italia.

Christian Eriksen alikuwa amehusishwa na tetesi za kuondoka Inter Milan mwezi Januari lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 anasema anafurahi kuwa katika klabu hiyo ya Serie A.

 

Tetesi zinasema Chelsea inahitaji angalau euro milioni 20 kumpata mlinzi wa Italia Emerson Palmieri,26, lakini Inter Milan na Napoli pia zinataka kumsajili.

Tetesi zinasema Manchester United iko tayari kutoa mkataba mpya kwa Ole Gunner Solskjaer kwasababu wa sasa hivi unakamilika baadaye mwezi huu.

Tetesi zinasema Barcelona inataka kumuuza mchezaji wa Brazil Philippe Coutinho, 28, ili iweze kulipa Liverpool deni lililosalia kutoka uhamisho wake wa mwaka 2018.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Watakua wamefanya poa sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Vinzur

    Jibu

    Ziko poa

    Jibu

    Itakuwa vizuri sana

    Jibu

    Ziko poa

    Jibu

    Zmeeleweka

    Jibu

    Ziko poaa

    Jibu

Acha ujumbe