Tetesi za soka Barani Ulaya leo Jumamosi Mei 08, 2021 zinasema:-
Tetesi zinasema, Barcelona wameanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, ambayo mkataba wake Manchester City unamalizika msimu huu. 

Tetesi zinasema, Kuteuliwa kwa Jose Mourinho kama mkufunzi wa Roma msimu ujao huenda kukamfanya kiungo wa kati wa Italia Lorenzo Pellegrini, 24, kuhamia Liverpool, baada ya meneja wa klabu hiyo kuonesha nia ya kuwaleta wachezaji aanaowajua, miongoni mwao mchezaji wa kimataifa wa Serbia na Manchester United Nemanja Matic, 32.
Tetesi za SokaTetesi zinasema, Mourinho pia ana matumaini ya kuungana tena na kipa wa Manchester United na Uhispania David De Gea, 30, baada kuchukua usukani Roma.

Tetesi zinasema, Wachezajiwa Real Madrid wanahofia meneja wao Mfaransa Zinedine Zidane, 48, “amechoka na kukasirika” na huenda akaondoka klabu hiyo kabla ya kukamilisha mwaka wa mwisho katika kandarasi yake msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Arsenal wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma, 24, huku Tottenham, West Ham na Everton pia zikimuulizia.

Tetesi zinasema, Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Mali Bissouma, baada ya kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsaka Declan Rice, 22 wa West Ham’.

Tetesi zinasema, Manchester United wameambiwa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mreno Andre Silva, 25, anagharimu £35m msimu huu.
Tetesi za soka- Eintracht FrankfurtTetesi zinasema, Chelsea utawauza walinzi wake kukusanya fedha za kuwanunua wachezaji wengine, wanaopigiwa upatu kuondoka Stamford Bridge ni Marcos Alonso, 30, na Emerson Palmieri, 26.

Tetesi zinasema, Atletico Madrid wanamnyatia kiungo wa kati wa Barcelona aliye na umri wa chini ya miaka 21-Mhispania Riqui Puigmsimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Barcelona na Paris Saint-Germain wanamfuatilia mlinzi wa wa Monaco kutoka Brazili Caio Henrique,23.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

tetesi za soka, Tetesi za Soka Barani Ulaya, Meridianbet

SOMA ZAIDI

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa