Tetesi zinasema Chelsea na Manchester City wanataka kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 32, kutoka Bayern Munich.

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameongeza mkataba wa muda wake Paris St-Germain Jana Jumamosi, hatua itakayomfanya kusalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2026.

Tetesi zinasema Real Madrid wamechoshwa na Eden Hazard na wako tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa Ubelgiji aliye na umri wa miaka 30 msimu huu wa joto.

 

Hazard Kuwakosa Atalanta Sababu ya Majeraha

Mkufunzi ajaye wa Roma boss Jose Mourinho ana mpango wa kubisha hodi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United kwa lengo la kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24.

Tetesi zinasema Tottenham Hotspur haina mpango wa kupokea ofa zozote za kumuuza mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema Aston Villa wanajiandaa kuwasilisha dau la £15m kumnunua winga wa Burnley wa chini ya miaka 21- Muingereza Dwight McNeil.

Tetesi zinasema Leicester City wanataka kuzipiku Liverpool na West Ham United katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard 23.

Mawakala wa Georginio Wijnaldum wanasema kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 30, angependelea kuzungumza na Bayern Munich kuhusu uhamisho wa bure baada ya kandarasi yake kumalizika Liverpool msimu huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Arsenal wanatathmini uwezekano wa kumnunua kipa Ajax na Cameroon Andre Onana,25, lakini watasubiri uamuzi wa rufaa ya marufuku ya dawa za kututumua misuli michezoni dhidi yake kabla ya kuwasilisha rasmi ofa yao.

Tetesi zinasema Tottenham na West Ham ni miongoni mwa klabu za Ulaya zinazomfuatilia mshambuliaji wa Besiktas na Canada Cyle Larin, 26.

Tetesi zinasema Everton wanataka kumsajili mlinzi wa Wigan Athletic James Carragher,18, ambaye ni mtoto wa kiume wa mchezaji mkongwe wa Liverpool Jamie.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa