Tetesi zinasema Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anatajwa kuwa mshabiki mkubwa wa kiungo wa Liverpool Naby Keita, 26, na anapenda kumuongeza mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea katika kikosi chake.

Tetesi zinasema Leicester City wanavutiwa na kumsajili mlinzi wa kushoto wa Southampton Ryan Bertrand ambaye mkataba wake unakwisha mwishoni mwa msimu huu.

Manchester United inaanda dau la pauni million 68 kwa ajili ya kiungo Marcos Llorente, wa Atletico Madrid, huku timu hiyo wakitaka kuharakisha mchakato wa kumsainisha mkataba mpya kiungo huyo ili aendelee kusalia katika klabu hiyo.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Mlinzi wa Kati RB Leipzig’s Dayot Upamecano, 22, ambae atajiunga na mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich baada ya ligi kumalizika, amesema alikataa nafasi ya kusajiliwa na Manchester United alipokuwa na miaka 17.

Klabu ya Tottenham inamatumaini ya kumshawishi beki Joachim Andersen, ambae msimu amekitumikia kikosi cha Fulham akitoea Lyon ya Ufaransa kuijiunga nao kuliko wapinzani wao wa kaskazini mwa London Arsenal.

Tetesi zinasema Leeds United wako mbele ya AC Milan katika mbio za kumsajili kiungo wa miaka 26 Rodrigo De Paul,wa Udinese, lakini pia Liverpool nao wanavutiwa na muargentina huyo.

Mchambuzi na nyota wa zamani wa Arsenal Ian Wright haamini kama Arsenal inapaswa kumsajili moja kwa moja kiungo Dani Ceballos, mchezaji anayecheza kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea Real Madrid.

Mlinda lango wa Wolves Mreno Rui Patricio, 33, ambaye amebakiza zaidi ya miezi 12 kwenye mkataba wake wa sasa na vijana wa Molineux, anaweza mlengwa kuu wa meneja mpya wa As Roma Jose Mourinho.

 

Xavi Atwaa Taji la Kwanza na Al Sadd SC.

Kiungo wa zamani wa Barcelona Xavi amesaini mkataba mpya ya kuendelea kuifundisha klabu ya Al-Sadd ya Qatar hadi 2023, Kuongeza mkataba kwa Xavi ni pigo kwa rais wa Barca Joan Laporta, ambaye anatafuta kocha wa kuchukua nafasi ya bosi wa sasa Ronald Koeman.

Tetesi zinasema Mama mzazi wa Cristiano Ronaldo, Dolores Aveiro, angependa mtoto wake huyo anarejea katika klabu ya Sporting Lisbon, ya Ureno iwapo mchezaji huyo ataondoka katika kabu ya Juventus.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa