Tetesi zinasema kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anamtaka mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, lakini the Blues wanahofu kuwa mahasimu wao wa magharibi mwa London watakataa kumtoa.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Tony Cascarino ameidokezea Tottenham kumfukuzia mshambuliaji wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 25 Ollie Watkins kuchukua nafasi ya Kane endapo ataondoka Spurs.

Tetesi zinasema Leeds United wamekubali kuingia mkataba mpya wa mwaka mmoja na kocha wao raia wa Argentina Marcelo Bielsa mwenye umri wa miaka 65, huku tangazo rasmi likitarajiwa kutolewa wiki hii.

 

Marcelo Bielsa

Tetesi zinasema klabu ya Manchester United inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wake wa zamani Cristiano Ronaldo aliyepo Juventus.

Tetesi zinasema Liverpool ina matumaini ya kumsajili kiungo wa Mali Yves Bissouma mwenye umri wa miaka 24 kutoka Brighton, Arsenal pia wanamuwania mchezaji huyo.

Paris St-Germain ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, ambaye anaondoka Liverpool kama mchezaji huru. Barcelona bado hawajaweka dau kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema klabu hiyo itaanza mazungumzo na Real Madrid kuhusu mkataba mpya kwa ajili ya kiungo wa kati anayecheza kwa mkopo Martin Odegaard, 22, katika wiki chache zijazo.

 

Odegaard

Tetesi zinasema Kiungo mchezeshaji wa Manchester United, Juan Mata hana uhakika kama ataendelea kusalia katika klabu hiyo baada ya kuisha kwa mkataba wake katika majira ya joto ya mwaka huu.

Arsenal wamekuwa wakihusishwa na mchezaji wa kikosi cha Roma cha vijana walio chini ya umri wa miaka 23 Cengiz ambaye amekuwa akicheza kwa mkopo msimu huu katika klabu Leicester City.

Meneja wa Norwich City Daniel Farke anasema atahitaji kuchukua mwelekeo wa hatari zaidi kuliko klabu nyingine katika soko la uhamisho iwapo wanataka kusalia katika Ligi ya Primia msimu ujao.

Barcelona wamekuwa na nia ya kumchukua kiungo wa nyuma-kushoto wa Atalanta na Ujerumani Robin Gosens, 26, ambaye amekuwa akihusishwa pia na Manchester City, Inter Milan, Juventus na AC Milan.

 

Zidane

Tetesi zinasema Zinedine Zidane atafanya maziungumzao na Real Madrid katika siku zijazo kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo.

Real Madrid wataangalia jinsi ya kumuuza kiungo wa safu ya kati Muhispania Dani Ceballos msimu huu, lakini Arsenal hawatataka mkataba wa kudumu kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 24.

Bournemouth wanataka kuendelea kuwa na mlinzi wa Marekani Cameron Carter-Vickers, 23, kwa mkataba wa kudumu baada ya mkataba wake wa mkopo kuisha Tottenham, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Newcastle United na Anderlecht.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa