Tetesi za soka zinasema, Kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte, ambaye ameachana na klabu ya Inter Milan jumatano wiki hii anataka kujiunga na klabu ya Tottenham.
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anajiandaa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Old Trafford, licha ya United kupoteza mechi ya fainali ya kombe la dhidi ya Villarreal.
Tetesi zinasema Klabu ya Juventus inatarajiwa kumfuta kazi kocha wao Andrea Pirlo na kumrejesha kocha wao wa zamani Massimiliano Allegri. Allegri anaweza kusaini mkataba na Juventus ndani ya saa 24 zijazo.
Klabu ya Real Madrid ilikuwa ikimpigia hesabu Allegri kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane, ambaye amejiuzulu kuinoa klabu hiyo jana Alhamisi. Madrid sasa wanatarajiwa kuhamishia nguvu zao katika kumsaka kocha wa PSG Paris St-Germain Mauricio Pochettino.
Tetesi zinasema Simone Inzaghi anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa Inter Milan baada ya kuachana na klabu ya Lazio.
Kocha wa zamani wa Tottenham Jose Mourinho anataka kiungo wa Uswizi na Arsenal Granit Xhaka, 28, kuwa mchezaji wa kwanza kumsajili katika klabu ya Roma.
Arsenal wanatazamiwa kutaka kulipwa dau la pauni milioni 21.5 kwa ajili ya Xhaka – lakini Roma wanaamini watalipa kitita kisichozidi pauni milioni 10.
Tetesi zinasema kumfuta kazi kocha Ronald Koeman kutawagharimu Barcelona takribani pauni milioni 12.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Juve wanaangaika sana inatakiwa wapate kocha bora wa kuwasaidia timu yao
Huu ni wakati wa Mauricio Pochettino kupiga mkwanja
Hatarii
Ziko poa tetesi