Tetesi zinasema, Manchester United wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo huku klabu hiyo ya Italia ikiwa iko tayari kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 36 kwa kubadilishana na kiungo wa kati Paul Pogba, 28.

Tottenham wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 24, ambapo itashuhudia kubadilishana na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane,27, pamoja na nyongeza ya fedha.

Tetesi zinasema, kiungo wa kati Dani Ceballos, 24, amesema anataka kusalia Real Madrid msimu ujao au kuondoka kabisa kwenye klabu baada ya kutumia misimu miwili akichezea klabu ya Arsenal.

Dani Ceballos

Tetesi zinasema Burnley wamepanga kutoa zabuni ya pauni milioni 10 kwaajili ya mlinzi wa kati Joe Worrall,24.

Kocha wa zamani wa England ma Crystal Palace yuko kwenye orodha ya kuchukua nafasi ya ukufunzi kwenye klabu ya West Brom baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce.

Tetesi zinasema, Tottehnam wana mpango wa kuanza mazungumzo rasmi na Paris St-Germain siku ya Jumatatu ukiwa mpango wa kumrejesha Mauricio Pochettino kwenye klabu.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Tottenham Steven Bergwijn anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa joto huku Ajax ikiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo, 23.

 

Tetesi zinasema, Aston villa wana hofu ya kumpoteza kiungo wao nyota Douglas Luiz ,23, huku timu yake ya zamani ya Manchester City ikihitaji kumsajili tena Mbrazili huyo.

Tetesi zinasema, AC Milan wataanza mazungumzo na Chelsea Jumatatu kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa England Fikayo Tomori,23 kwa mkataba wa kudumu.

Arsenal imemwambia kocha wa Roma Jose Mourinho kuwa wanahitaji pauni milioni 17 kwa ajili ya kiungo wa kati Granit Xhaka, 28.

West Ham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Mzambia Patson Daka wanapotafuta namna ya kuziba nafasi ya Sebastian Haller. Mchezaji huyo wa miaka 22 pia amevutiwa na Liverpool, Manchester United na Manchester City.

Tetesi zinasema, Leeds hawana mpango tena wa kumnyakua kiungo wa kati wa Liverpool Harry Wilson msimu huu wa joto.

 

 

Mwenyekiti wa Brighton Tony Bloom yuko tayari kusikiliza ofa za wachezaji kama kiungo wa Mali Yves Bissouma, 24, na mlinzi wa Kiingereza Ben White, 23, huku wakizivutia Arsenal, Liverpool na Manchester United.

Tetesi zinasema, Southampton wana mpango kumsajili kiungo wa Everton Tom Davies baada ya mwaka jana kushindwa kumsajili Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22.

Mchezaji wa Manchester United Diogo Dalot amekiri kuwa hajui mustakabali wake baada ya kiungo huyo wa kati,22, kucheza kwa mkopo AC Milan msimu uliopita.


 

MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa