Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Chelsea wako tayari kumsajili tena mshambuliaji wa Inter Milan Rumelu Lukaku msimu huu wa joto huku klabu hiyo ya Italia ikiwa imejiandaa kusikiliza ofa kwa ajili ya Mbelgiji huyo wa miaka 28.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wana nia ya kuendelea kubaki na Mauricio Pochettino kama kocha wa klabu hiyo wakati Real Madrid wakijiunga na Tottenham katika kumnasa mkufunzi huyo.

Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka ,28, amesema anashawishiwa na kocha wa Roma Jose Mourinho, lakini ana furaha kuichezea klabu ya jijini London.

 

Ningesepa Juventus....

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala anajiandaa kufanya mazungumzo mapya na Juventus, huku kocha mpya Massimiliano Allegri akiwa na shauku na mustakabali wa kudumu na mchezaji huyo, 27, baada ya kurejea Turin.

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Saul Niguez, 26, atashinikiza kuhamia Manchester United mbele ya Juventus au Paris St-Germain katika dirisha la usajili la majira ya joto.

Tetesi zinasema, mlinzi Thiago Silva anajiandaa kusalia Chelsea kwa msimu mwingine baada ya mchezaji huyo, 36, kuisaidia timu yake kupata ushindi wa ligi ya mabingwa.

 

Silva Kuwakosa United Darajani.

Hatua ya Arsenal kumchukua mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 18 wa Sporting Lisbon Tiago Tomas iko katika mizani baada ya Gunners kushindwa kufuzu Uropa.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Villarreal Mhispania Gerard Moreno, 29, anazivutia West Ham, Newcastle na Roma.

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Tottenham Serge Aurier,28, amesema anajiandaa kuachana na klabu hiyo, msimu huu wa joto huku PSG na AC Milan zikiwa timu zinazovutiwa na mchezaji huyo.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Lukaku arudi tu Chelsea maana kumenoga

    Jibu

    Ziko vizuri

    Jibu

Acha ujumbe