Tetesi zinasema, Real Madrid watamsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, anayekipiga Paris St-Germain, huku mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi ,28, akitoka PSG kwenda Juve.

Jose Mourinho aliwasiliana na Real Madrid wiki iliyopita, kabla ya kumteua Carlo Anclotti kuwa kocha wa klabu hiyo, pamoja na kocha huyo wa zamani wa Real na Tottenham kukubali kuwa mkufunzi wa Roma mwezi uliopita.

Tetesi zinasema, matumaini ya Chelsea ya kupata saini ya Romelu Lukaku yamegonga mwamba baada ya mchezaji huyo, 28, mshambuliaji wa Kibelgiji kusema kuwa anasalia Inter Milan.

 

Lukaku Inter

Barcelona bado wako kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay,27, kuhusu uhamisho wa bure kutoka Lyon, huku kiungo wa kati Georginio Wijnaldum,30, atajiunga kwa uhamisho wa bure kutoka Liverpool.

Tetesi zinasema, Manchester United wamerejesha nia yao ya kumsajili beki wa kulia Kieran Trippier,30, kutoka Atletico Madrid.

Aston Villa ni moja kati ya klabu 12 za ligi ya primia zinazopanga uhamisho wa mshambuliaji Chris Wood na Burnley itataka takribani pauni milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Tetesi zinasema, West Ham na New York City wametangaza ofa kwa mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud,34, anayejiandaa kuondoka Chelsea kwa uhamisho wa bure.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Kocha wa Real Madrid Carlos Ancelotti amesema kuwa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,31, na mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard,30 , bado mustakabali wao unaweza kuwa bado uko kwenye klabu hiyo.

Kiungo wa kati wa Borussia Monchenglabach, Florian Neuhaus,24, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool amekana taarifa kuwa amefikia makubaliano kujiunga na Bayern Munich.

Tetesi zinasema Arsenal, Manchester United na Tottenham wote wameonesha nia ya kumpata beki wa kulia wa Lille Mturuki Zeki Celik,24.

Tetesi zinasema West Ham na Southampton wanachuana kumsajili mlinzi wa Barcelona Junior Firpo,24.

Tetesi zinasema West Ham wako kwenye hatua za juu za mazungumzo kumnasa Alex Kral,23, kutoka Spartak Moscow kwa zaidi ya pauni milioni 20.

Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero,33, alikataa ofa kutoka Juventus kujiunga nao na kuchagua kujiunga na Barcelona kwa uhamisho wa bure akitokea Manchester City.

 

Kane

Tetesi zinasema Sevilla wanapenda kumsajili mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez,32, kutoka Inter Milan.

Leeds United wana nia ya kumnasa beki wa kushoto wa Uhispania anayekipiga Huesca Javi Galan,26, ambaye kipengele chake cha uhamisho katika mkataba wake kimeshuka mpaka pauni milioni 3.5.

Tetesi zinasema West Brom wanajiandaa kupata kocha mpya baada ya mazungumzo na kocha wa zamani wa Sheffield United Chris Wilder,53.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa