Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, ameieleza Crystal Palace kwamba anataka kuondoka kabla ya msimu wa mazoezi kuanza.

Kocha mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti yuko tayari kumtafuta aliyekuwa mshambuliaji wa iliyokuwa klabu yake Everton raia wa Brazil Richarlison, 24.

Tetesi zinasema Everton iko tayari kutoa ofa ya mkataba wa miaka mitatu kwa aliyekuwa kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo, 47.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Arsenal na Aston Villa wametenga rasmi vitita vyao kwa winga wa Argentina anayechezea Norwich anayesemekana kwamba thamani yake ni pauni milioni 40 Emi Buendia, 24.

Barcelona inasemekana kuwa tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Ilaix Moriba, 18, licha ya timu za Manchester United, Manchester City na Chelsea kuonesha nia ya kumsaka.

Liverpool inaongoza katika mbio za kumsajili winga Raphinha kutoka Leeds lakini Manchester United na Manchester City pia nazo zina msaka mchezaji huyo Mbrazil, 24.

Tetesi zinasema Arsenal iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 22, kwa euro milioni 10 sawa na (£8.6m) pekee.

Tetesi zinasema Ajax imeipiku Manchester United katika kumsajili winga wa Ghana Kamaldeen Sulemana, 19, kutoka FC Nordsjaelland.

Tetesi zinasema Olivier Giroud, 34, yuko tayari kuichagua AC Milan mkataba wa mshambuliaji huyo wa Chelsea raia wa Ufaransa utakapokamilika.

 

Inter Yaingia Mazima kwa Giroud.

Sead Kolasinac, 27, kutoka Bosnia yuko tayari kuuzwa na Arsenal baada ya Schalke kusema haikuweza kubadilisha mkataba wa mkopo wa beki huyo wa kushota kuwa wa kudumu msimu huu.

Tetesi zinasema Atletico Madrid iko tayari kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26, ambaye awali aliwahi kuhusishwa na Manchester United.

Tetesi zinasema Fiorentina ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 26, kwa mkopo kutoka Chelsea msimu huu.

Kocha anayerejea Massimiliano Allegri alikutana na wafanyakazi wa Juventus Alhamisi, huku hatma ya mshambuliaji raia wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, ikiwa kipaumbele katika orodha ya ajenda zake.

Tottenham bado inafanya mazungumzo na mshambuliaji wa Korea Kusini Heung-min Son, 28, kuhusu mkataba wake mpya na ina imani ya kufikiwa kwa makubaliano punde tu kocha wao mpya atakapochaguliwa.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Douglas Luiz anatarajiwa kusalia na Aston Villa kwasababu Manchester City haina uwezekano mkubwa wa kuzingatia kipengele cha kumnunua tena kiungo huyo wa kati Mbrazil, 23.

Tetesi zinasema Kocha wa Atletico Madrid raia wa Argentina Diego Simeone, 51, anakaribia kukubali kuongezwa mkataba wa miaka miwili hadi mwaka 2024.

Tetesi zinasema Mabingwa Ufaransa Lille inataka kumtangaza Patrick Vieira, 44, kama mrithi wa aliyekuwa kocha wa timu timu hiyo Christophe Galtier.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa