Tetesi zinasema, Iwapo mazungumzo ya kumsajili winga wa England na Borrusia Dortmund Jadon Sancho ,21 yatagonga mwamba , Manchester United huenda ikamwinda Hudson Odoi , Dembele au Christiano Ronaldo.36.
Iwapo Chelsea itamsaini Hakimi basi wanaweza kusikiza ofa za kumuuza winga wa England Hudson Odoi 20 au Tino Livramento, huku Aston Villa ikihusishwa.
Tetesi zinasema, Paris St-Germain inachunguza hali ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo ya Barcelona imesalia mwaka mmoja.
Barcelona inafikiria kumsajili winga wa England na Manchester City Raheem Sterling ambaye anaonekana kama chaguo la kuchukua nafasi yake Dembele iwapo hataongeza kandarasi yake.
Tetesi zinasema, Meneja wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anawania umeneja wa Everton baada ya kazi hiyo kuachwa wazi.
Mmiliki wa klabu ya Inter Miami Jorge Mas amethibitisha kwamba yeye na mmiliki mwenza wa klabu hiyo David Beckham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji Muargentina Lionel Messi, 33, kuhusu kujiunga na timu hiyo.
Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameweka sharti aliposaini mkataba mpya na PSG kwamba hawatamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, msimu huu.
Tottenham wanafanya mazungumzo na winga wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Marcus Thuram mwana wa kiume wa mshindi wa Kombe la Dunia Lillian kabla ya uwezekano wa uhamisho msimu wa majira ya joto.
Mkurugenzi ajaye wa michezo Fabio Paratici atamuambia Harry Winks kwamba Tottenham itasikiliza ofa kwa ajili ya kiungo huyo wa kati Muingereza mwenye umri wa miaka , 25, msimu huu.
Kiungo wa safu ya kati wa timu ya Ujerumani ya RB Leipzig Muaustria Marcel Sabitzer, 27, ambaye awali alihusishwa na taarifa za kuhamia klabu ya Tottenham, anataka kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga na anaweza kuondoka kwa mauzo ya pauni milioni 15 msimu huu.
Tetesi zinasema, Burnley wamekubali mkataba mpya na meneja Sean Dyche, 49, ambaye anatarajiwa kusaidiwa katika kipindi cha dirisha la uhamisho la msimu wa majira ya joto.
Tetesi zinasema huenda meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard akarejea kazini lakini mara hii katika klabu ya Crystal Palace baada ya mazungumzo na meneja wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo kugonga mwamba.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
magdalena
United nao wanayumba