Tetesi zinasema, Jadon Sancho, 21, atakuwa ndiye mchezaji wa pili atakayelipwa zaidi Manchester United, nyuma ya mlinda lango David de Gea, iwapo atakamilisha uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund msimu huu.

Tetesi zinasema, meneja wa zamani Roma Paulo Fonseca amekubali kimsingi kanuni ya mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuifunza timu ya Tottenham.

Tetesi zinasema, Liverpool wako katika mazungumzo na Borussia Monchengladbach kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mjerumani Florian Neuhaus, 24.

Tetesi zinasema, Arsenal wanajiandaa kwa ajili ya kumsajili beki wa Brighton na England Ben White, mwenye umri wa miaka 23.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Chelsea wanamtaka kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez, 26, lakini Manchester United na Juventus zimesalia kuwa ndio timu ambazo mchezaji huyo anazipendelea zaidi.

Sevilla wamempatia beki mhispania Sergio Ramos, 35, mkataba wa miaka mitano. Mkataba wa Ramos pale Real Madrid unaisha msimu huu.

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 32, yuko huru kuondoka Bayern Munich.

Everton wanaangalia uwezekano wa kusajili Mcroashia Nikola Vlasic, 23, anayecheza katika safu ya mashambulizi kutoka CSKA Moscow – miaka miwili baada ya kumuuza.

Tetesi zinasema, Beki wa wa England Danny Rose, 30, anakaribia kujiunga na Watford baada ya kuondoka Tottenham.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema Beki wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 28, amekubaliana kuhusu masharti ya binafsi na klabu ya Paris St-Germain.

Mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 22, anakaribia kukamilisha mkataba huru wa uhamisho kwenda Paris St-Germain. Ataondoka AC Milan msimu huu wakati mkataba wake utakapokwisha.

Mkataba wa kiungo wa kati wa England Jude Bellingham utaongezwa katika Dortmund utaongezwa mara moja kwa miaka miwili zaidi hadi 2025 atakapotimiza umri wa miaka 18 baadaye mwezi huu.

Tetesi zinasema, Arsenal wameanzisha mazungumzo na mlinzi wa Uskochi Kieran Tierney, 24, juu ya kurefushwa kwa mkataba wale.

Burnley wameweka dau la pauni milioni 12 kwa ajili ya mlinzi wa timu ya Stoke na Jamuhuru ya Ireland Nathan Collins, mwenye umri wa miaka 20.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Arsenal watazidisha nia yao kumchukua kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 24,msimu huu.

Tetesi zinasema, Besiktas wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa Sevilla na Uholanzi Luuk de Jong, 30.

Fulham wamekataa dau la pauni milioni 16 kutoka kwa klabu ya Urusi ya Dynamo Moscow kwa ajili ya mshambuliaji Mserbia Aleksandar Mitrovic, 26.

Barcelona walifanya mkataba na meneja Mjerumani Joachim Low mapema mwaka huu kabla ya kuthibitisha kuwa Ronald Koeman ataendelea kuwa meneja wao.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa