Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Aston Villa wanaamini watasalia na kiungo wao wa kati Jack Grealish,25, ambaye ananyatiwa na Manchester City, Chelsea na Manchester United.

Tetesi zinasema, Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Brighton kuhusu mkataba wa mlinzi wa Uingereza Ben White, 23, ambao huenda ukawa wa thamani ya zaidi ya pauni milioni 50.

Tetesi zinasema, Dean Smith hana mpango wa kumuuza kiungo wa kati wa Scotland John McGinn, 26, msimu huu wajoto, huku Liverpool ikihusishwa kumsajili.

 

Liverpool imeanza mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusu mkataba wa mshambuliaji wa Uholanzi Donyell Malen, 22, ambaye anatarajiwa kugharimu karibu pauni milioni 34.

Tetesi zinasema, Brighton, Burnley, West Ham na Norwich City iliyopandishwa daraja hivi karibuni wamehusishwa na mshambulzi wa Barcelona na Denmark Martin Braithwaite,30.

West Ham wamewasilisha dau la pauni milioni 17 kumnunua mlinzi wa Fiorentina aliye na umri wa miaka 23- Nikola Milenkovic, lakini ofa hiyo iko chini ya kiwango cha fedha kinachotakiwa na klabu hiyo ya Serie A kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia.

Tetesi zinasema, Burnley wanajiandaa kuwasilisha dau la kumnunua kipa wa kimataifa wa Werder Bremen na Jamhuri ya Czech Jiri Pavlenka, 29.

Tetesi zinasema, Crystal Palace wamemgeukia kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre katika juhudi zao za kumsaka meneja mpya.

 

Hata hivyo, Favre anahofia kukubali nafasi ya pale Selhurst Park kwasababu ya bajeti ndogo ya klabu hiyo kununua wachezaji wapya.

Leeds United huenda wakamnunua mshambuliaji wa Blackburn Rovers Ben Brereton,22, baada ya kufanya vizuri na Chile katika michuano ya Copa America.

Rafael Benitez bado anaongoza katika kinyang’anyiro cha ukufunzi wa Everton, huku kocha wa zamani wa Liverpool akifanya mazungumzo zaidi na Toffees juu ya kumrithi Carlo Ancelotti.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe