Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema,mchezaji wa Manchester City na England, Raheem Sterling yuko tayari kuondoka klabuni hapo. Lakini meneja Pep Guardiola anataka winga huyo mwenye umri wa miaka 26 kubakia Etihad, licha ya Real Madrid kuonyesha kumuhitaji.

Gareth Bale, 31, anaweza kustaafu kucheza soka la klabu mara baada ya mkataba wake mnono na Real Madrid anaolipwa £600,000 kwa wiki utakapokoma msimu ujao.

Crystal Palace imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, muingereza Morgan Rogers, 18. Kocha mpya wa klabu hiyo Patrick Vieira anataka kuboresha na kuweka sawa uwiano wa umri katika kiosi hicho msimu huu.

 

Tetesi zinasema, Kiungo wa England Kalvin Phillips, 25, ana furaha kwenye klabu yake ya Leeds United na hana mpango wa kuikacha klabu hiyo ya Elland Road, kwa mujibu wa wakala wake.

Klabu za Chelsea na Arsenal zinamfuatilia mlinzi wa Bayer Leverkusen na Burkina Faso Edmond Tapsoba. Lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna ofa ya uhakika na rasmi iliyowasilishwa kwake.

Tetesi zinasema, Aston Villa inaamini kwamba inaweza kumpata kiungo wa Arsenal Emile Smith Rowe na watawasilisha dau jingine la tatu kwa ajili ya muingereza huyo.

Tetesi zinasema, Arsenal inaendelea kumshawishi mlinzi wa Brighton Ben White, 23, ambapo tayari imeshawasilisha dau la £50m kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

 

Tetesi zinasema, Burnley wanamtaka mlinda mlango wa Wales Wayne Hennessey, 34 ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Crystal Palace. Chelsea na Aston Villa pia wanahusishwa naye.

Barcelona itawapa nafasi Chelsea ya kumsajili mshambuliaji wake Antoine Griezmann. Magwiji hao wa Catalan wanaokabiliwa na tatizo la kifedha wanataka kumpiga bei mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 30 ili kukamilisha mkataba mpya wa Lionel Messi.

Tetesi zinasema, Manchester United na Arsenal wanataka kumsajili mlinzi wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27 anaonekana kutokwenda sawa na mipango ya meneja Ronald Koeman.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe