Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Tottenham inaweza kuwa tayari kumuachilia kiungo wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, katika makubaliano ya kubadilishana na raia mwenzake mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial.

Tetesi zinasema, Liverpool bado inaweza kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa West Ham Jarrod Bowen. Walihusishwa na ofa ya pauni milioni 20 kwenye dirisha la majira ya joto.

Borussia Dortmund inaweza kuwasilisha ombi la kumajili winga wa Juventus na Italia Federico Chiesa, 23, endapo klabu hiyo ya Bundesliga itampoteza mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, msimu ujao wa joto.

 

Federico Chiesa
Federico Chiesa

Liverpool pia imejiunga na mbio za kusaji Haaland wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke akikiri itakuwa vigumu kusalia na nyota huyo msimu ujao wa joto.

Kiungo wa kati wa Real Madrid ya Uhispania Marco Asensio, 25, pia ni miongoni mwa wanaolengwa na Liverpool.

Meneja wa Ureno Paulo Fonseca, 48, anasema hatua yake ya kuisimamia Tottenham ilitibuka kwa sababu mkurugenzi wa michezo Fabio Paratici alitaka Spurs icheze mpira wa kujilinda.

Tetesi zinasema, Mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, hatakimbilia uamuzi juu ya maisha yake ya baadaye, lakini anataka nyongeza ya mshahara ikiwa atasalia Stamford Bridge.

 

Meneja wa Bayern Munich Julian Nagelsmann anasema bado hajazungumza na mkurugenzi wa michezo Hasan Salihamidzic kumhusu Rudiger, ambaye hana mkataba mpya mwaka ujao.

Arsenal inatarajiwa kumpoteza mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette bure wakati mkataba wake utamalizika msimu wa joto, na Atletico Madrid inavutiwa na mchezaji huyo wa miaka 30.

Tetesi zinasema, Manchester United wamefanya mawasiliano na Barcelona juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa 24 Ousmane Dembele.


FUNGA BAHATI YAKO NA MERIDIANBET.

Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe