Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Real Madrid watamkosa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland,21, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kujiunga na Manchester City, Paris St-Germain au Bayern Munich.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund wamekasirishwa na kitendo cha kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel kuzungumza hadharani kuhusu nia ya klabu yake ya kumsajili Haaland.

Tetesi zinasema, Everton wanamtaka kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, mwezi Januari.

 

Jesse Lingard

Barcelona inataka kuishinda Real Madrid katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, ambaye mkataba wake unamalizika msimu unaokuja.

Tetesi zinasema, Kiungo wa Manchester United, Donny van de Beek, 24, hatarudi Ajax lakini kuna nafasi kubwa kwamba ataondoka Old Trafford.

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema klabu hiyo haijapokea ofa kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wake wa Uholanzi Van de Beek, licha ya uwepo wa taarifa nyingi.

 

Liverpool, Manchester United na PSG walimpa ofa ya pesa nyingi Ansu Fati ili ajiunge nazo kabla ya kinda huyo mwenye miaka 18 mzaliwa wa Guinea-Bissau, mchezaji wa kimataifa wa Hispania kusaini mkataba mpya Barcelona.

Mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini anasema ingekuwa bora mshambuliaji wa Ureno wa Cristiano Ronaldo, 36, kuondoka Juve na kujiunga na Manchester United mapema zaidi.

Tetesi zinasema, Kiungo wa zamami wa Arsenal na England Jack Wilshere, 29, yuko tayari kuhamia ligi kuu ya Marekani kujiunga na klabu ya Inter Miami.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe