Tetesi zinasema Liverpool wamewasiliana na miamba wa Ujerumani Bayern Munich kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 29.

Hata hivyo, Reds hawana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Vasco da Gama Mbrazil Talles Magno, licha ya tetesi zinazomhusisha kiungo huyo wa miaka 18- kuhamia Anfield.

Mkuu wa soka wa Borussia Dortmund, Sebastian Kehl, amethibitisha kuwa mshambuliaji wa England Jadon Sancho,20, atasalia katika klabu hiyo licha ya kwamba ananyatiwa na Manchester United.

 

Tetesi za Soka barani Ulaya.

Tetesi zinasema United wako tayari kumenyana na Chelsea katika kinyang’anyiro cha kusajili beki wa kushoto wa Leicester City na England Ben Chilwell, 23.

Kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak,27, anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusiana na hatima yake katika klabu hiyo japo Chelsea wanamtaka.

Arsenal watatangaza usajili wa wa kiungo wa kimataifa wa Brazil Willian, 32, kwa mkataba wa miaka mitatu wikendi hii baada ya mkataba wa mshambulaji huyo kukamilika Chelsea.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Kocha mpya wa Juventus Andrea Pirlo amemewafahamisha mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 32, na kiungo wa kati wa Ujereumani Sami Khedira, 33, kwamba wapo huru kuondoka klabu hiyo msimu huu wa jotor.

Tetesi zinasema Manchester United na Tottenham huenda wakapewa nafasi nyingine ya kumsaini mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 26, kutoka Juventus msimu huu wa joto.

United itaitisha £20m kutoka kwa Roma ambayo inataka kumsajili beki wake wa safu ya kati na nyuma mwenye umri wa miaka 30- Chris Smalling, amabye yuko tayari kupunguziwa mshahara kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Italia Serie A.

Napoli wako tayari kuafikiana na Everton kuhusu mkataba wa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Allan, 29.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

West Ham wanataka zaidi ya £80m kumuuza kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21, licha ya kiungo huyo kutakiwa na Chelsea.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Rudi Voller inasisitiza kuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz, anayenyatiwa na Chelsea, ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo chini ya makubaliano maalum.

Beki wa Chelsea na Italia Emerson Palmieri, 26, amefikia mkataba wa kibinafsi na klabu ya Inter Milan.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Chelsea wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsaini beki wa kushoto wa Real Madrid Mhispania Sergio Reguilon, 23, kujiandaa kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

41 MAONI

  1. ntasikitika sana kama nited hawatomchukua sancho maana amekuwa ni mchezaji mzuri sana na pale united yule mzee anazingua sana bora tu atolewe maana maamuzi yake katika sakata la kununua wachezaji amekuwa akizingua sana na ndo maana timu inashuka viwango vyake tofauti na awali

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa