Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Meneja wa Paris St-Germain na raia wa Argentine Mauricio Pochettino anapigiwa upatu na klabu ya Man United ili kuchukua mikoba ya Solskjaer msimu ujao.

Tetesi zinasema, meneja wa Ajax Ten Hag amekanusha uvumi wa kuhusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester United, akisema ajapata ombi lolote kutoka katika klabu hiyo.

Wakala wa Kireno Jorge Mendes anaisukuma Man United kujaza pengo la Ole Gunnar Solksjaer kwa kumuajiri meneja wa Sevilla Julen Lopetegui. Raia huyo wa Uhispania ana kandarasi na klabu hiyo hadi 2024.

 

mount

Tetesi zinasema, Real Madrid inataka kumsajili kiungo wa Chelsea na England Mason Mount. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo katika mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya.

Mkufunzi mpya wa klabu ya Aston Villa Steven Gerrard anataka kumsajili beki wa kushoto wa Croatia Borna Barisic, 29, kutoka klabu yake ya zamani Rangers.

Mkufunzi wa Everton, Rafael Benitez anasema kwamba klabu hiyo itahitaji kusajili wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku winga wa England Demarai Gray, 25, akipata jeraha wakati wa mechi waliopoteza dhidi ya Manchester City.

 

Messi

Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi, 34, hana mpango wa kurudi Barcelona baada ya rais wa klabu hiyo Joan laporta kusema kwamba klabu hiyo ya Uhispania inaweza kumsajili raia huyo wa Argentina majira ya kiangazi.

Tetesi zinasema, Meneja mpya wa Barcelona, Xavi anataka kumsajili mshambuliaji wa Algeria Baghdad Bounedjah ,29 kutoka klabu ya zamani ya Al-Sadd nchini Qatar.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

CHEZA HAPA

Acha ujumbe