Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Manchester United wanataka kumtoa kwa mkataba wa mkopo kiungo Mholanzi Donny van de Beek, 24, kwa Newcastle au Borussia Dortmund.

Tetesi zinasema, Manchester United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 25.

Mshambulizi wa West Ham Jarrod Bowen anataka kuhamia Liverpool, ambao bado wana nia ya kutaka kumnunua Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 25.

Tetesi zinasema, Newcastle wameongeza juhudi kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Muingereza Todd Cantwell, 23. The Magpies pia wamewasilisha ombi rasmi la kumnunua beki wa Sevilla, Diego Carlos, 28.

 

Tetesi zinasema, Newcastle wameambiwa watahitaji kulipa zaidi ya £37m kumsajili beki wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic, 24.

Tottenham wanatazamia kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, kwa klabu za Italia, huku Juventus wakiwa na uwezekano mkubwa zaidi.

Southampton wanatarajia kufanya mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa kimataifa wa Albania Armando Broja kutoka Chelsea kuwa wa kudumu.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25.

Jurgen Klopp anatarajia mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 26, kusalia Liverpool baada ya dirisha la uhamisho la Januari.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Arsenal wana orodha ya wachezaji saba wanaolengwa na wachezaji kama vile Youri Tielemans wa Leicester, 24, Georginio Wijnaldum wa Paris St-Germain, 31, na Bruno Guimaraes wa Lyon, 24.

Tetesi zinasema, Aston Villa wameonyesha nia ya kutaka kumnunua mlinda lango wa Paris St-Germain raia wa Uhispania Sergio Rico, 28.

Watford, Southampton na Norwich wanamfuatilia winga wa Lewes Ollie Tanner mwenye umri wa miaka 19.

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anatumai kufanya uhamisho wa mkopo wa winga wa Uingereza Ademola Lookman kutoka RB Leipzig kuwa wa kudumu.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe