Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Winga wa Barcelona Ousmane Dembele, 24 anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ili kujiunga na Manchester United au Juventus huku Chelsea na Bayern Munich wakiwa wametupwa nje katika harakati za kumsaini mchezaji huyo.

Newcastle United inafikiria kuwasilisha ombi la kutaka kumsajili kipa wa klabu ya PSG Keylor Navas lakini klabu hiyo ya Ligue 1 inataka kumdhibiti kipa huyo mwenye umri wa miaka 35 raia wa Costa Rica na kwamba hawako tayari aondoke.

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, amekataa ombi la yeye kujiunga na klabu ya Newcastle kwa mkopo kutokana na nafasi ilio klabu hiyo katika jedwali la ligi ya premia.

 

Tetesi zinasema, Newcastle inapiga hatua katika majaribio yao ya kutaka kumsajili beki wa Sevilla na Brazil mwenye umri wa miaka 28 Diego Carlos.

Tetesi zinasema, Chelsea ina hamu ya kumsajili beki wa PSG raia wa Ufaransa Layvin Kurzawa, 29, kwa mkopo lakini mazungumzo hayajaanza kati yao.

Southampton ipo katika mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa kudumu wa raia wa Alabania ambaye anahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo , 20, Armando Broja.

Arsenal imewasilisha ombi la pauni 50m ili kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, huku ikimuuza kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ili kupunguza gharama ya mchezaji huyo.

 

Arsenal bado ina hamu ya kumsajili beki wa kulia wa Nottingham Forest aliyepo kwa mkopo Djed Spence lakini mchezaji huyo wa Middlesborough , 21, pia anavutia hamu kutoka kwa vigogo wa Italia Roma na Inter Milan.

Juventus inamnyatia kiungo wa kati wa Arsenal na raia wa Ghana Thomas Partey, 28, kushirikishwa katika mkataba wowote wa klabu hiyo ya serie A wa kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 25.

Tetesi zinasema, Leicester City inajiandaa kuondoka kwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24. Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji huyo ikiwaimesalia na miezi 18 katika kandarasi yake.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe