Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Manchester City wako tayari kuipiku Real Madrid katika kumsajili mshambuliaji wa River Plate Julian Alvarez. Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 21 amepewa jina la Sergio Aguero mpya.

Newcastle United wana matumaini ya kumsajili beki wa Burnley James Tarkowski, huku Burnley wakiwa tayari kuchukua ofa ya kumnunua Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 29.

Wawakilishi wa mlinzi wa Sevilla Diego Carlos wanajaribu kuishawishi klabu hiyo kumuuza kwa Newcastle. The Magpies wanamtaka Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 28, huku klabu hiyo ya Uhispania ikitaka takriban pauni milioni 60.

 

Arsenal wamewasilisha ombi la euro milioni 70m (£58.6m) kumnunua mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic. Mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao 17 katika mechi 21 za Serie A msimu huu.

Tetesi zinasema, West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, lakini Everton inataka pauni milioni 60 kwaajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

Burnley wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus Aaron Ramsey, 31, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Kocha Massimiliano Allegri amethibitisha kuwa Mchezaji huyo wa Wales ataondoka katika klabu hiyo mwezi Januari.

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anasema Eden Hazard yuko mbioni kusalia katika klabu hiyo. Winga huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 31 amehusishwa na kurejea Ligi ya primia Januari hii.

Tetesi zinasema, Aston Villa wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Juventus mwenye umri wa miaka 24 Rodrigo Bentancur. Mchezaji huyo, raia wa Uruguay amecheza mechi 18 za Serie A msimu huu.

Tetesi zinasema, West Ham wamejiondoa kwenye mbio za kumsajili winga wa Wolves Adama Traore baada ya kuambiwa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 25 anasaini kwenda Tottenham.

 

Chelsea wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua mlinzi wa kushoto wa Stuttgart Borna Sosa, 24. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia alilengwa na Aston Villa mapema wakati wa dirisha la usajili, huku Inter Milan pia ikimtaka.

Liverpool wamejiweka kando katika kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Denis Zakaria. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 25 awali alihusishwa na kuhamia Anfield.

Tetesi zinasema, Atletico Madrid wanataka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso. Mhispania huyo, 31, anasemekana kulengwa na timu hiyo ya La Liga.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe