Tetesi zinasema, Barcelona na Juventus wamewasilisha ombi rasmi la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang 32 kwa mkopo kwa kipindi cha msimu kilichosalia.

Meneja wa West Ham, David Moyes anafaikiria kumsajili mshambuliaji wa Leeds, Raphina na ana mpango wa kumnunua kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari kufungwa.

Winga wa England Raheem Sterling anatarajiwa kuendelea na mazungumzo ya kuandikisha kandarasi mpya na Manchester City. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 unaisha 2023 na Barcelona, PSG na Real Madrid zina hamu ya kumsajili.

 

Eriksen

Brentford wanatarajia kutangaza usajili wa mchezaji wa Denmark Christian Eriksen wikendi hii. Mchezaji huyo aliwekwa kidhibiti moyo bada ya kuzimia wakati wa michezo ya Euro 2020 mwezi Juni.

Mchezaji wa Wales Aaron Ramsey huenda atasalia katika klabu ya Juventus baada ya kukataa uhamisho wa kuelekea Aston Villa, Burnley, Crystal Palace, Newcastle United na Wolves mwezi huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Everton inataka kumsajili Kiungo wa kati wa England Ruben Loftus Cheek kutoka Chelsea.

Tetesi zinasema dau la Aston Villa la £20.8m kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Uruguay Rodrigo Bentancur limekataliwa na Juventus.

Juventus ina mpango wa kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho, 30 ambaye kandarasi yake katika klabu ya Chelsea inakamilika 2023.

Monaco inataka kati ya Yuro 80m na 100m kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni, ambaye anatakiwa Real Madrid huku Chelsea na Manchester United pia zikimnyatia.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa