Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anapanga mazungumzo na wakala wake kuhusu mustakabali wake wa Manchester United baada ya kukatishwa tamaa na maisha huko Old Trafford.

Mlinda mlango wa Chelsea mwenye thamani ya pauni milioni 72 Kepa Arrizabalaga, 27, anaweza kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto huku The Blues wakiwa hawajapanga kumzuia mchezaji huyo wa Uhispania ikiwa anataka kuondoka.


Tetesi zinasema, Barcelona wameshinda mbio za kumsajili kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia analengwa na Liverpool.

 

Franck Kessie Apewa Ofa ya Mkataba Spurs

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, 29, yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo ya Anfield huku Barcelona na Real Madrid wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal.

Leicester City wamepunguza dau la kumnasa Youri Tielemans, 24, kutoka pauni milioni 60 hadi pauni milioni 35, huku Arsenal na Manchester United wakiwa katika mbio za kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji msimu huu.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu huu kunaweza kuwa muhimu katika kumfunga winga wa Uingereza Bukayo Saka, 20 ambaye anahusishwa na Liverpool.

Tetesi zinasema, Meneja wa Uhispania Luis Enrique, 51, ameibuka kuwa mgombea wa kushtukiza kwenye kibarua cha kocha wa Manchester United.

 

Mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta anataka kuzungumza na Chelsea kuhusu mustakabali wake, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akihusishwa na kuhamia Barcelona mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto.

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal Alexis Sanchez, 33, anatazamiwa kuongezewa mkataba mpya na Inter Milan, lakini raia huyo wa Chile atalazimika kukatwa mshahara.

Tetesi zinasema, Arsenal wamekamilisha usajili wa mlinda mlango Mmarekani Matt Turner mwenye umri wa miaka 27 kutoka New England Revolution kwa pauni milioni 7.5.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa