Tetesi zinasema, Chelsea inaangalia usajili wa mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, kama kipaumbele chake wakati wa usajili wa majira ya joto Declan Rice, 23, na Aurelien Tchouameni, 22 wanahusishwa pia.

Meneja wa Leicester, Brendan Rodgers anasema timu hiyo inapaswa kuwa wa kweli kuhusu hatma ya kiungo wake wa kimataifa wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24, ambaye anaingia katika miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake akihusishwa na klabu za Arsenal na Manchester United.

 

Tielemans Hana Mapango wa Kuendelea Kusalia Leicester

Arsenal inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Armando Broja, 20 wakati wa majira ya joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Albania kwa sasa anafanya vyema akiwa kwa mkopo na klabu ya Southampton.

Tetesi zinasema, Juventus wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kiungo mfaransa Adrien Rabiot, 26, na mlinzi wa kushoto Mbrazil Alex Sandro, 31.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 22, anasakwa na vilabu vya Arsenal na Newcastle katika dirisha lijalo la usajili.

 

Paris

Tetesi zinasema, Mauricio Pochettino anafikiria kuondoka Paris St-Germain msimu huu baada ya kutofautiana na baadhi ya maafisa waandamizi wa klabu hiyo.

Manchester United inamuwania mlinzi wa Borussia Monchengladbach Ramy Bensebaini, 26, ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria kuziba nafasi ya mlinzi wa kushoto wa England Luke Shaw.

Pep Guardiola anataka Raheem Sterling, 27, asaini mkataba mpya kusalia Manchester City lakini anasema klabu hiyo itakua na uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya mshambuliaji huyo wa England.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa