Tetesi zinasema, Kiungo mfaransa Paul Pogba, 28, yuko tayari kupokea ofa kutoka klabu zingine za ligi kuu England wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Newcastle inajiandaa kutoa ofa ya £45m kwa ajili ya kiungo mchezeshaji wa Crystal Palace muingereza Eberechi Eze, 23.

Nyota wa Manchester United Jesse Lingard, 29 anaweza kukataa kuhamia Tottenham bure mwishoni mwa msimu, kiungo huyo mshambuliaji wa England angetamani kucheza nje ya nchi hiyo.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet
Jesse Lingard.

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amegusia kwamba klabu hiyo huenda ikamsajili moja kwa moja kutoka kwenye mkopo kiungo mfaransa Tanguy Ndombele, 25 kutoka Tottenham kama klabu hiyo itatwaa kombe la Europa League.

Winga wa Brazil wa Leeds United Raphinha, 25 ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool, amekataa kusaini mkataba mpya kusalia katika klabu yake hiyo ya Elland Road.

Tetesi zinasema, Arsenal ni timu ya hivi karibuni ya ligi kuu England kuonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji mreno wa AC Milan Rafael Leao, 22.

Newcastle inakabiliwa na mtihani wa kumbakiza mlinzi wake kutoka Uswiswi Fabian Schar, 30 ambaye mkataba wake unaingia katika miezi ya mwisho huku AC Milan, Sevilla na Valencia zikimtaka.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Brendan Rodgers anasema nyota wa Leicester City Wilfred Ndidi ana thamani kubwa zaidi ya £50m baada ya Aston Villa kuhusishwa na kiungo huyo wa Nigeria,25 msimu huu.

Tetesi zinasema, Manchester United wanavutiwa kumsajili winga mbrazil wa Ajax Antony, 21 ambaye huenda akaungana na kocha Erik ten Hag pale Old Trafford kama uhamisho huo utazaa matunda.

West Ham imeungana na Leeds katika mbio za kumsaka kiungo muingereza wa Huddersfield Lewis O’Brien, 23 mwenye kipengele cha thamani ya £12m kwenye mkataba wake.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa