Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema Paris St-Germain na Manchester United wanapigiwa upatu kumsajili Lionel Messi baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 33, kuifahamisha Barcelona kwamba anataka kuondoka, wako tayari kulipa ada ya kumpata.

Barua iliotumwa na klabu hiyo siku ya Jumanne inasema kwamba anataka kutumia kifungu kilichopo katika kandarasi yake ili kuweza kuondoka katika klabu hiyo akiwa mchezaji huru mara moja.

Barcelona ilifungwa magoli 8-2 na klabu ya Ujerumani ya Bayern katika robo fainali ya kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mnamo tarehe 16 Agosti.

Barcelona hata hivyo inaamini kwamba kifungu hicho kilipitwa na wakati na kwamba kandarasi ya Messi katika klabu hiyo itakamilika 2021 huku kukiwa na kifungu cha Yuro milioni 700 kwa klabu yoyote inayotaka kumnunua.

Thiago Silva, 35, yuko tayari kufanyiwa vipimo vya matibabu na Chelsea siku ya Alhamisi, licha ya jaribio la dakika za mwisho za Paris St-Germain kutaka kumpatia mkataba mpya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.
Thiago Silva

Philippe Coutinho angelipendelea kurejea katika Ligi ya Epl badala ya Barcelona huku Manchester United, Arsenal na Chelsea wakimnyatia nyota huyo wa Brazil aliye na umri wa miaka 28.

Everton wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid James Rodriguez, 29, baada ya mkufunzi Zinedine kuonesha ishara ya kumtaka aondoke klabu hiyo.

Chelsea wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili mlinzi wa zamani wa Nice Malang Sarr, 21, kwa mkataba wa miaka mitano.

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek yuko tayari kuhamia Ligi ya Epl msimu huu wa joto huku Manchester United wakiwa mbioni kumsaka Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23.

Tetesi zinasema Newcastle United wanamtaka mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Arsenal Rob Holding, 24, kwa mkopo na Gunners wako tayari kupokea ofa.

Tetesi zinasema AC Milan wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid Mhispania Brahim Diaz, 21, kwa mkopo msimu wa 2020-21.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Crystal Palace wamekubali kulipa £14m kumnunua kiungo wa kati wa QPR Eberichi Eze, baada ya kuzidisha dau lililowasilishwa kuchelewa na West Brom kumpata mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 22- Fulham walijiondoa.

Tetesi zinasema Aston Villa, Leeds United na West brom pia wanamsaka Watkins.

Everton, Leicester City, Southampton na Leeds United wamewatuma wasaka vipaji wao kufuatilia mchezo wa kiungo wa safu ya kati na nyuma wa Dundee United Lewis Neilson, 17.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

41 Komentara

    Barcelona sasa inaelekea pabaya mana wachezaji wenye uwezo wa kuifikisha timu mbali wanataka kuondoka inakuwa hatari sana

    Jibu

    daaa itakuwa vizuri sana abadilishe mazingira

    Jibu

    Sio mbaya atakuwa anabadilisha mazingira#Meridianbettz

    Jibu

    Bora aende akaangalie upepo mwingine

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Messi na Philippe Coutinho ni wachezaji bora ambao itakua vizuri Philippe Coutinho kurudi tena kwenye viunga vya Uingereza wakati Messi nae aje kuonyesha cheche zake pale Uingereza ili kunogesha kidogo EPL

    Jibu

    Ni Jambo zuri m2 kutoka sehemu moja kwenda nyingine

    Jibu

    Barcelona wana halingumu sana hadi kukamilisha kikosi chao kuna kazi ya ziada

    Jibu

    Sidhani Kama Messi ataondoka Barcelona

    Jibu

    Ni bora akabadilishe upepo

    Jibu

    Man wanamutaji sana messi ila sijui kama mwenyewwe atakubali kiacha barcelona

    Jibu

    Bora akabadili mazingira mana amekaa sana barcelona

    Jibu

    Messi ni bora haende man u itakuwa poa sana

    Jibu

    Hii ni habari njema

    Jibu

    Mashabiki tunashukuru kwa taarifa
    @meridianbettz

    Jibu

    Aende abadili upepo

    Jibu

    Messi hawezi kuondoka barcelona maana akiondoka itakuaje

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Chelsea imepata beki wa viwango vyake

    Jibu

    Naona ni sawa tu akabadili mazingira

    Jibu

    Itakuwa habari nzuri kama messi ataondoka

    Jibu

    Thiago Silva ni beki kiongozi ingawa umri wake mkubwa#meridianbettz

    Jibu

    Habari njema Sana

    Jibu

    Zimekaa vizuri sana.

    Jibu

    Sasa kwa Barca itakuwa hatar I km wachezaji wazur wakisepa timi itaxid kulega.

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Popote kambi mrad mkono uende kinywan

    Jibu

    Waswahil tunasema adui wako muombee njaa atakuheshim tu ata Kama alikuwa shujaa upande wang nimejifunza hilo maana usajil wa Messi kwenda PSG kutawafanya wakae vzur pia inatakiwa ndo wakae wajipange vzur Barcelona kwa hilo

    Jibu

    Messi ni wa Barcelona tu!!

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Messi atasepa tu barca

    Jibu

    Apo vilabu wajimaliz kushawish

    Jibu

    Hizi zimekaa poa.

    Jibu

    Duu Barcelona kimenuka Hari yahewa imetibuka Sasa mwisho wabarcelona nikushuka kimpila nawatu wakiondoka itabaki Barcelona jina sasa

    Jibu

    Messi kaipiga pigo kubwa sana Barcelona maana pengo lake bado hawakutafuta mbadala

    Jibu

    Habari njema.

    Jibu

    Messi na Philippe Coutinho ni wachezaji bora ambao itakua vizuri Philippe Coutinho kurudi tena kwenye viunga vya Uingereza wakati Messi nae aje kuonyesha cheche zake pale Uingereza ili kunogesha kidogo EPL

    Jibu

    messi na coutinho ingependeza sana wangekuja united #meridianbet

    Jibu

    Messi nae atupe break kidogo

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Hizi bado ni tetesi tu

    Jibu

Acha ujumbe