Tetesi zinasema, Real Madrid bado wana uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, kwa uhamisho wa bila malipo kutoka Paris St-Germain na wanapanga kutangaza mkataba huo mwishoni mwa msimu huu.

Tetesi zinasema, Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 22, kutoka kwa mabingwa wa Uhispania Atletico Madrid.

Mshambulizi wa Manchester United wa Uruguay Edinson Cavani, 35, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, anasemekana kuwa tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu ya Botafogo ya Brazil.

 

Edinson Cavani

Tetesi zinasema, Christopher Nkunku atagharimu Manchester United angalau Euro 75m ikiwa wataendelea na juhudi za kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24.

Tetesi zinasema, Newcastle na Aston Villa wangeongoza mbio za kumnasa Joe Gomez iwapo Liverpool itaamua kumuuza mlinzi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 msimu huu.

Tottenham wamejitokeza na ofa thabiti zaidi ya kutaka kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala, 28, kutoka Juventus msimu wa joto, lakini Barcelona na Inter Milan zinasalia kuwa chaguo la Muargentina huyo.

Crystal Palace wanakabiliwa na pambano la kutaka kumbakisha mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 18, Michael Olise, 20, ambaye anasakwa na Arsenal, Chelsea na Everton pamoja na Bayern Munich na Lille.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Liverpool wanatarajiwa kuanzisha upya nia ya kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 24, ambaye ana thamani ya Euro 90m.

Tetesi zinasema, Arsenal wako tayari kumpa meneja Mikel Arteta mkataba mpya wa miaka mitatu msimu huu wenye thamani ya £25m.

Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Savio kutoka Atletico Mineiro, kabla ya kumpeleka kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 kwa PSV Eindhoven.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa