Tetesi zinasema, Manchester United wana uhakika wa kufikia malengo yao ya uhamisho msimu huu wa joto hata kama watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, huku kiungo wa kati wa West Ham ya Uingereza Declan Rice, 23, na mshambuliaji wa Tottenham, 28, Harry Kane, akiwa kwenye orodha yao.

Chelsea na Paris St-Germain wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake wa Barcelona utakapokamilika msimu huu wa joto.

 

Ousmane Dembele Aachwa Kwenye Kikosi cha Barca

Arsenal wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad na Uswidi Alexander Isak, 22, ambaye ni mmoja wa walengwa wakuu wa mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, West Ham wamechagua kuongeza kandarasi ya mlinzi wa pembeni wa Uingereza Ben Johnson,22, hadi mwaka 2024 ili kuzuia uwezekano wa kutakiwa na Arsenal, Tottenham na Liverpool

Tetesi zinasema, Spurs wanavutiwa na mlinda mlango wa Athletic Bilbao na Uhispania Unai Simon, 24, huku wakifikiria kuhusu mbadala wa muda mrefu wa Mfaransa Hugo Lloris, 35.

Leicester City wanaweza kufufua nia yao ya kumnunua winga wa Italia Domenico Berardi ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ataamua kuondoka Sassuolo inayoshiriki Serie A msimu huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

West Bromwich Albion wanamlenga kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, 24, ambaye alicheza chini ya kocha wa Baggies Steve Bruce katika klabu ya Newcastle United.

Tetesi zinasema, Meneja wa zamani wa Hull City Grant McCann, 41, amekubali dili la kuwa meneja wa klabu ya Championship Peterborough United.

Tottenham wako tayari kumuuza Steven Bergwijn msimu huu wa joto huku AC Milan wakimtaka winga huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa