Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Liverpool inamtaka winga wa Villarreal na Uholanzi Arnaut Danjuma, 25, kuchukua nafasi ya mshambuliaji Sadio Mane, lakini Liverpool haina mpango huo kwa sasa hadi mwaka 2023.

Kama kocha wa Ajax Erik ten Hag akichaguliwa kuwa meneja wa Manchester United kama invyotarajiwa, basi atamsajili kiungo wa kati wa Portugal Ruben Neves, 25, Kutoka Wolves.

Tetesi zinasema, Wakala wa mchezaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26, yupo nchini Italia akikutana na AC Milan, Juventus na Atalanta.

 

Tuchel Ametupilia Mbali Uvumi Kuhusu Hatima ya Werner

Paul Pogba , 29, anapendelea kurudi Juventus kuliko kwenda Paris St-Germain baada ya muda wake kuisha majira ya joto.

Tetesi zinasema, Arsenal, Everton na Newcastle wote wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay kutoka Barcelona.

Winga wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo, 22, ameweka wazi mapenzi yake kwa Arsenal huku akiendelea kuuhusishwa na vilabu vingine ikiwemo Manchester United na Liverpool.

Tetesi zinasema, viongozi wa ngazi za juu huko Inter Milan sasa wanataka mshambuliaji wa Chelsea na Belgium Romelu Lukaku (28) arudi klabuni hapo.

Brighton hawana mpango wa kumuuza kipa wake Sanchez mbali ya kuwa Newcastle wameonesha nia ya kumuhitaji kipa huyo Mhispania (24).

 

Lewandowski

Tetesi zinasema, Barcelona ina nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, msimu huu wa majira ya joto.

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Ryan Gravenberch, 19, amekubali kuingia mkataba binafsi na Bayern Munich.

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, anaweza kutia Saini mkataba mpya katika klabu yake ya Paris St-Germain mbali na kuonesha nia kwa Real Madrid.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe