Tetesi zinasema, Paris St-Germain wanahusishwa katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku, 28 mwaka mmoja tu baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kuwagharimu Blues pauni milioni 98 kutoka Inter Milan.
Manchester United na Arsenal wamejiunga na mbio za kumsajili, mshambuliaji wa Benfica, Darwin Nunez baada ya kutuma mawakala wake kumfuatilia katika mchezo wa wikiendi hii.
Tetesi zinasema, Roma wanataka kumsajili kiungo wakati wa Aston Villa Mbrazili Douglas Luiz, 23, msimu huu.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland, 21, ameachana na nia ya kujiunga na klabu ya Manchester United kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway haamini kuwa anaweza kutimiza ndoto zake Old Trafford
Roma, AC Milan na Juventus wamejiunga na West Ham na Newcastle katika nia ya kumsajili mshambuliaji wa Jesse Lingard, 29, wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika msimu huu.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund ndio wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji Mbelgiji Eden Hazard, 31, kutoka Real Madrid wakiungana na Arsenal na AC Milan.
Chelsea wamewasiliana na mshambuliaji wa akademi ya Arsenal ya Khayon Muingereza Edwards juu ya uwezekano wa uhamisho, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 akiwa bado hajaamua mkataba wa kikazi na Gunners.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.