Tetesi zinasema, Liverpool imekubali kumlipa mshambuliaji Mohamed Salah pauni 400,000 kwa wiki ili kumshawishi nahodha huyo wa Misri kubaki Anfield.

Tetesi zinasema, Corinthians, Botafogo na Flamengo wamewasiliana na nahodha wa Manchester City Fernandinho kuhusu uhamisho wa msimu ujao baada ya tangazo la kushitukiza la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 la kuondoka Etihad.

West Ham wameingia katika mbio za kumsaka winga wa Bayer Leverkusen Moussa Diaby. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22 pia anafuatiliwa na Liverpool kama mchezaji anayeweza kumrithi salah, iwapo ataondoka.

 

Bale Bado Anaiwaza Ligi Kuu Epl.

Tetesi zinasema, Tottenham na Cardiff wamejiunga na klabu zinazotaka kumsajili mshambuliaji kutoka Wales Gareth Bale, 32, wakati mkataba wake wa Real Madrid utakapoisha mwezi Juni.

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City na Uhispania Spain David Silva anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Real Sociedad, lakini klabu hiyo inataka apunguziwe mshahara.

Tetesi zinasema, Manchester City wanakabiliwa na ushindani wakati wanapoendela kumfuatilia kiungo wa River Plate Muargentina Enzo Fernandez, 21.

Aberdeen wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kumchukua mlinda lango wa klabu ya Ipswich Town mwenye umri wa miaka 31 kutoka Czech Vaclav Hladky, ambaye awali alicheza chini ya Dons boss Jim Goodwin akiwa St Mirren.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Arsenal na Newcastle zinahusishwa na kiungo wa Lyon, Lucas Paqueta, 24. Mchezaji huyo wa kimataifa wa The Brazil awali alihusishwa na taarifa za kuhamia Paris St-Germain, gharama yake ni pauni milioni 58.

Tetesi zinasema, Newcastle wako tayari kumsajili mlinzi kutoka Ireland mwenye umri wa miaka 17- Alex Murphy kutoka klabu ya Galway United.

Meneja wa Rangers, Giovanni van Bronckhorst anataka kumleta mshambuliaji wa Sunderland na Scotland Ross Stewart, 25, kutua Ibrox.

Tetesi zinasema, Arsenal wanaandaa ofa ya euro milioni 20 (£16.6m) kwa ajili ya winga Mturuki kutoka Galatasaray Kerem Aktürkoğlu mwenye umri wa miaka 23.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa