Tetesi zinasema, Newcastle wametoa kwa Benfica euro 60m (£50m) kwa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 22, kujaribu kuwapiku wapinzani wa Ligi ya Premier wanaowania kumsajili.

Kocha Maurizio Sarri anatamani kuungana tena na Jorginho huko Lazio, huku kiungo huyo wa kati wa Italia, 30, akiwa hana uwezekano wa kupewa kandarasi mpya na Chelsea baada ya 2023.

Anaetarajiwa kuwa Meneja mpya Manchester United, Erik ten Hag anamtaka kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 22 anapendelea kuondoka Ligue 1 mwishoni mwa msimu.

Van Gaal: Ten Hag Kuwa Makini Man United ni Klabu ya Biashara

Tetesi zinasema, Arsenal, Leeds na Newcastle wanachuana kumsajili kiungo wa kati wa Hoffenheim na Austria Florian Grillitsch, 26, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto.

Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, anataka kusalia Leeds na atakataa ombi la Manchester United kwa kusaini mkataba mpya.

Tottenham watakuwa kwenye soko la kutafuta beki wa kati wa upande wa kushoto msimu huu wa joto na wanafuatilia hali ya mlinzi wa Uhispania Mario Hermoso, 26, huko Atletico Madrid.

Borussia Dortmund wameafikia makubaliano ya maneno na Red Bull Salzburg kuhusu kumsajili Karim Adeyemi lakini fowadi huyo wa Ujerumani, 20, bado yuko kwenye mazungumzo na Liverpool, RB Leipzig na Paris St-Germain.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Kipa chaguo la pili wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, 27, anawaniwa na Juventus.

Barcelona wameongeza kasi katika kumsaka nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 32, huku beki huyo wa Uhispania akishinikiza kuondoka huku kukiwa na hali ya sintofahamu ya kifedha huko Stamford Bridge.

Paolo Dybala, 28, anapanga kufanya mazungumzo na Arsenal na Tottenham huku kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Argentina katika klabu ya Juventus ikitarajiwa kumalizika msimu wa joto.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa