Tetesi zinasema, Arsenal inamtaka mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 25, na tayari mkurugenzi wa ufundi wa Gunners ameshafanya mazungumzo na wawakikishi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Paris St-Germain imempa mshambuliaji mfaransa Kylian Mbappe, 23, mkataba wenye thamani ya £42m kwa mwaka, utakaomfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.

Tetesi zinasema, Kocha wa Tottenham Antonio Conte anataka kuinoa PSG msimu ujao akiwa na uhakika wa kurithi mikoba ya kocha wa zamani wa Spurs Mauricio Pochettino pale Parc des Princes.


 

Antonio Conte

Newcastle wanajiandaa kumsajili mlinda mlango wa PSG Keylor Navas, ambaye ataondoka lakini mkongwe huyo wa Costa Rica, mwenye miaka 35 anawaniwa pia na Juventus na Sevilla.

Declan Rice amekataa kwa mara ya tatu ofa ya mkataba mpya kutoka West Ham wenye mshahara wa £200k kwa wiki. Licha ya klabu hiyo kusisitiza kwamba kiungo huyo wa England hauzwi.

Tetesi zinasema, Tottenham imewasiliana na Inter Milan kuhusu kumsajili mlinzi wa kulia wa Uholanzi Denzel Dumfries, 26.

Celtic wako katika mazungumzo ya mwisho na Tottenham kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kati wa Marekani Cameron Carter-Vickers, 24, kwa uhamisho wa kudumu.

Tetesi zinasema, Newcastle wanamfuatilia mlinzi wa Monaco mfaransa, Benoit Badiashile, 21, na winga wa Bayer Leverkusen mfaransa Moussa Diaby, 22.

 

Rooney Amkejeli Christiano Ronaldo

Wayne Rooney amekataa ofa ya kufanya kazi kama msaidizi wa Erik ten Hag pale Manchester United, akisisitiza kwamba ataondoka tu Derby County akipata ofa ya kuwa meneja na sio msaidizi.

Tetesi zinasema, Fulham inataka kumsajili kiungo wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, pale Craven Cottage.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa