Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 30, anatakiwa na meneja mpya wa Manchester United Erik ten Hag. Eriksen anacheza Brentford kwa mkataba wa miezi sita ambao utamalizika mwisho wa msimu huu.

Arsenal wanapania kufufua nia yao ya kumsaka mshambuliaji wa Uinngereza Tammy Abraham, 24, msimu huu wa joto na watatoa ofa ya £50m kwa Roma katika jaribio la kutaka kumsajili.

Tetesi zinasema, Real Madrid wanaongoza katika mbio ya kumsajili beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 29, ambaye anaondoka Chelsea mwisho wa msimu huu.

 

Antonio Rudiger

Mazungumzo kati ya wawakilishi wa Kylian Mbappe na Paris St-Germain kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji huyo wa miaka 23- yanaendelea vyema.

Kocha wa Barcelona Xavi anataka kusalia na kiungo wa kati wa Mholanzi Frenkie de Jong, 24, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United.

Tetesi zinasema, Leicester wanataka kumsajili kiungo wa kati wa PSV Eindhoven Ibrahim Sangare, 24. Bei ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast huenda ikawa £30m.

Tetesi zinasema, West Ham itajaribu kumsaini beki wa kati Michael Keane, 29, kutoka Everton ikiwa Toffees watashuka daraja katika Ligi ya Primia msimu huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Napoli wanataka angalau euro 80m (£67m) ikiwa wataamua kumuuza mshambuliaji wa umri wa miaka 23 Victor Osimhen, ambaye ni miongoni mwa walengwa wa Arsenal msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Rodrigo de Paul, 27, anataka kurejea Italia na anafuatiliwa na Inter Milan.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa