Tetesi zinasema, Manchester United wanataka kutoa £50m kwa ajili ya kiungo wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26, msimu ujao.

Borussia Dortmund itachuana na Manchester United kusaka saini ya mshambuliaji wa Ajax na Ivory Coast Sebastien Haller, 27.

Arsenal itafanya mazungumzo na nyota wake anayeshikilia rekodi ya uhamisho klabuni hapo Nicolas Pepe, 26, mwishoni mwa msimu kuhusu hatma ya winga huko wa Ivory Coast.

Barcelona inapambana kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, 33, lakini bado hawajapeleka ofa kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Poland.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 25, angetamani kutua Arsenal kuliko Newcastle.

Mshambuliaji wa zamani wa Everton James Rodriguez, 30, anataka kurejea Ulaya ambapo Mcolombia huyo itamlazimu kushusha mshahara wake kufanikisha hilo.

Roma inaitolea macho ligi kuu England msimu huu. Klabu hiyo ya Serie A inamtaka kiungo wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka, 29, kiungo wa Aston Villa Mbrazil Douglas Luiz, 23, na kiungo wa Manchester United Mserbia Nemanja Matic, 33.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Kiungo wa Liverpool na Hispania Thiago Alcantara, 31, awali alitakiwa na Manchester United kabla ya kutua Anfield, anasema Rio Ferdinand.

Unai Emery anataka kumsajili mshambuliaji wa Watford Mnigeria Emmanuel Dennis, 24, kumpeleka Villarreal katika dirisha la kiangazi.

 


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa