Tetesi zinasema, Manchester City inaamini Pep Guardiola atasaini mkataba mpya mwishoni mwa msimu, huku mazungumzo yakifanyika kuhusu kumuongezea Mhispania huyo muda wa kusalia City mpaka 2025.

Manchester City na Manchester United zinataka kumsajili kiungo wa England James Ward-Prowse kutoka Southampton, wakat Arsenal, Newcastle United na Tottenham zikifuatilia kwa karibu maendeleo ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ametangaziwa ofa nono kutoka klabu ya Paris St-Germain kuliko ile ya klabu yake ya Barcelona, lakini mwenyewe chaguo lake ni kusalia Nou Camp ambapo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Manchester City na Manchester United zinapigana vikumbo kuwania saini ya mlinzi wa kati wa Hispania, Pau Torres, 25, kutoka Villarreal.

Erik ten Hag, ambaye ataondoka Ajax kwenda kuwa meneja wa Manchester United mwishoni mwa msimu, anataka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Feyenoord na Uholanzi Tyrell Malacia, 22, kumpeleka katika klabu hiyo ya Old Trafford.

Kiungo mholanzi Frenkie de Jong amekuwa akihusishwa na klabu ya Manchester United lakini Bosi wa Barcelona Xavi anasema nyota huyo mwenye miaka 24 ni tegemeo la sasa na la baadaye la klabu hiyo ya Hispania.

Chelsea watamuongezea mkataba bora zaidi mlinzi wa kulia wa England Reece James, 22 ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid, mara itakapopata wamiliki wapya.

Tetesi zinasema, Real Madrid itawalazimu kutumia mpaka £33.5m kumrejesha mlinzi wa kushoto wa Hispania Sergio Reguilon, 25, kutoka Tottenham.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Wolves wako tayari kumuuza kiungo wake mreno Ruben Neves, 25 huku klabu hiyo ya West Midlands ikitarajia kuongeza nguvu katika kikosi chake kwa kusajili washambuliaji na viungo wapya.Crystal Palace, Watford na Fulham wanamfuatilia mlinzi wa FC Koln mjerumani Timo Hubers, 25 ambaye amekuwa akihusishwa pia na Leeds United.

Tetesi zinasema, Newcastle United imempa kiungo muingereza Sean Longstaff,24 mkataba wa miaka 4, mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, AC Milan imekubaliana na Lille kumsajili kiungo mreno Renato Sanches, 24, kwa ada ya £16.8m.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa