Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayekipiga Liverpool Sadio Mane, 30, ataiarifu klabu yake hiyo matamanio yake ya kuondoka msimu huu wa joto. Bayern Munich wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 34 kwa ajili ya kumsajili Mane.

Liverpool wamewasiliana na wawakilishi wa winga wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele, 25. Dembele pia anawindwa na Chelsea.

 

Ousmane Dembele, Kutoboa Nje ya Barca Kupo?

Beki wa Villarreal na Hispania Pau Torres, 25, anakaribia kuhamia Manchester United baada ya wakala wake kusafiri kwenda England kuendelea na mazungumzo ya uhamisho huo.

Tetesi zinasema, West Ham na Southampton wanafuatilia maendeleo ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Austria Junior Adamu mwenye umri wa miaka 20.

Arsenal wameiambia Benfica mlinda mlango wa Ujerumani Bernd Leno, 30, anapatikana kwa dau la £8.5m.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Leeds United raia wa Brazil Raphinha, 25, huenda akapendelea kuhamia Manchester United badala ya Barcelona.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tottenham wameiambia Villarreal kuwa wanataka pauni milioni 17 ili kumuuza kiungo wa kati wa Argentina Giovani Lo Celso, 26.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wanataka kumsajili mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, 25.

Barcelona wanavutiwa na mpango wa kuwasajili mlinzi wa Sevilla na Mfaransa Jules Kounde, 23, au mlinzi wa Napoli raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 30, kama beki mpya wa kati.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa