Tetesi zinasema, Chelsea wameanza mazungumzo na Sevilla kuhusu kumsajili beki wa Ufaransa mwenye thamani ya pauni milioni 50 Jules Kounde, 23.

Mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 29, yuko tayari kuondoka Liverpool na atasalia Ligi kuu ya uingereza endapo hatapewa mkataba mpya anaoutaka wa kusalia Reds.

Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30, anataka kuondoka Liverpool msimu huu wa joto, huku klabu ya Bayern Munich ikiwa na ushindani mkubwa katika kuiwania saini yake.

 

Mane Kuondoka Liverpool Msimu Huu.

Tetesi zinasema, Newcastle wako kwenye majadiliano juu ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Reims mwenye umri wa miaka 19 Mfaransa Hugo Ekitike katika mkataba wa pauni milioni 25.

Baada ya kutangaza kuachana na Paul Pogba na Jesse Lingard, Manchester United imeanza mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kuhusu uhamisho wa £72.5m kwenda Old Trafford.

Tetesi zinasema, Juventus wamekubali mpango wa kumrejesha Pogba, 29, wakati mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa na Manchester United utakapokamilika msimu huu.

 

Pogba

Wolves wanakaribia kumsajili Joao Palhinha wa Sporting Lisbon, huku kiungo huyo wa kati wa Ureno, 26, akikubali kujiunga kwa mkataba wa muda mrefu kwa ada ya takriban £20m.

Tetesi zinasema, Real Madrid wanamtaka kiungo wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, lakini hawatamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 hadi mwaka 2023.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa