Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Liverpool Msenegal Sadio Mane, 30, anasema atafanya kile ambacho watu wanataka alipokuwa akijibu kuhusu kura ya maoni nchini Senegal ambayo ilibaini kuwa 60-70% ya watu wanamtaka aondoke Liverpool.

Leeds United haitakubali dau la chini ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga wa Brazil Raphinha, 25, wambaye amekuwa akihusishwa sana na taarifa za kuhamia Barcelona.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Tottenham na nahodha wa England Harry Kane, 28, sasa anaweza kusaini mkataba mpya kubakia katika klabu hiyo.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Winga wa Tottenham Mholanzi Steven Bergwijn, 24, anasakwa na klabu ya Ajax, ambao wako tayari kumpatia mchezaji huyo wa zamani wa PSV Eindhoven mkataba mpaka mwaka 2027.

Tetesi zinasema, Tottenham na Chelsea wanashindania kusaini mkataba na mlinzi wa klabu za RB Leipzig Croatia Josko Gvardiol, 20.

AC Milan wanajiandaa kutangaza kusaini mkataba na mshambuliaji Mbelgiji Divock Origi, 27, ambaye amekwishaaga kuondoka Liverpool.

Tetesi zinasema, Aston Villa wanakamilisha taratibu za kusiani mkataba wa £2.8m na kipa wa Roma Mswidi Robin Olsen, 32, baada ya msimu wake wa mkopo kuisha msimu uliopita.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Mfaransa Corentin Tolisso, 27, anaweza kuhamia Ligi ya Primia wakati mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa mwezi Juni .

Tetesi zinasema, Mchezaji mwenye uzoefu wa Juventus na mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini, 37, yuko tayari kuhamia Marekani kusaini mkataba na Los Angeles FC.

Tetesi zinasema, Brentford wanajiandaa kumnunua mshambuliaji wa Watford Mnigeria Emmanuel Dennis mwenye umri wa miaka 24 kwa pauni milioni 20.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa